tiko
tiko
Wanafunzi wa
shule ya msingi Mail Kumi iliyopo halmashauri ya Mtwara vijijini
wanalazimika kusoma katika mazingira mabovu kutokana na bajeti ya fedha
iliyotakiwa kuongeza madarasa katika shule hiyo kupelekwa kwenye ujenzi
wa maabara.
ITV ilifika
katika shule ya msingi Mail Kumi na kujionea hali ilivyo ambapo mkuu wa
shule hiyo Mussa Mshangani anasema shule hiyo ina mikondo minne na
inawanafuzi 223 huku madarasa yakiwa mawili tu hali inayowalazimu baadhi
yao kusoma katika madarasa ya mbavu za mbwa.
Akizungumzia
changamoto hiyo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara vijijini Oscar
Ng’itu anasema lengo la halmashauri ni kuongeza madarasa lakini hilo
limeshindikana kutokana na sehemu kubwa ya vyanzo vya mapato kupelekwa
kwenye ujenzi wa maabara.
Hata hivyo
mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho saidi mchomeko anasema umasikini
lakini pia muitikio duni wa elimu katika kijiji cha maili kumi
unachangia wananchi kushindwa kujitolea ipasavyo katika ujenzi wa
madarasa.
-Itv
tiko
tiko
Post a Comment