tiko
tiko
Familia
ya Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima,
imeeleza hofu yake kwamba imeshangwazwa na hali ya afya ya kiongozi
huyo kubadilika ghafla akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi akihojiwa
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es
Salaam, mke wa Askofu Gwajima, Grace Gwajima, alisema familia bado
haielewi ni kwa namna gani Askofu huyo alizimia ghafla wakati aliondoka
nyumbani akiwa mzima wa afya.
Alisema
kama familia kuna vitu vinavyowachanganya na hawapati majibu haraka
ikiwamo la Askofu Gwajima kuondoka nyumbani akiwa mzima wa afya huku
akitembea, lakini muda mfupi baadaye anapelekwa hospitali akiwa amezimia
akihojiwa na polisi.
“Tunahisi
kuna kitu amefanyiwa, kwa maana haiwezekani mtu aondoke nyumbani akiwa
wa afya, lakini baadaye kidogo tunapewa taarifa amezimia yupo TMJ, hapa
kutakuwa na kitu,” alisema Grace akiwa na mmoja walinzi wa Askofu
Gwajima.
HALI YA ASKOFU GWAJIMA
Akizungumzia
hali ya Askofu Gwajima, aliyelazwa hospitalini hapo kwa siku tatu,
Grace alisema mumewe anaendelea vizuri na madaktari walikuwa wanajiandaa
kumtoa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) jana na
kumpeleka wodi ya wagonjwa wa kawaida.
Alisema
kwa sasa Askofu Gwajima anaweza kuongea, kula chakula na hata
kuzungumza na watu mbalimbali wanaofika kumjulia hali. “Kuna improvement
zimeaza kujitokeza, ki ukweli kuna hali ya uzima na anaendelea vizuri,”
alisema Grace.
Hata
hivyo, waandishi wa habari walizuiwa na uongozi wa Hospitali ya TMJ
kwenda kumwona Askofu Gwajima na badala yake walimwita Grace azungumze
na waandishi.
KUKAMATWA KWA WACHUNGAJI
Mke
wa Askofu Gwajima (Grace), alidai kuwa juzi usiku Polisi walifika
hospitalini hapo na kuwakamata wachungaji 30 waliofika kumjulia hali
Askofu Gwajima.
Alidai kuwa Polisi waliwakamata wachungaji hao pamoja na magari yao na kuwapeleka kusikojulikana.
“Jana
usiku kulizuka tafrani hapa hospitalini, Polisi walifika na kuwakamata
wachungaji wapatao 30 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na kuondoka nao,”
alidai Grace.
Hata
hivyo, Tulimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova, kuthibitisha taarifa hizo, lakini alisema angetuma
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, hadi tunakwenda
mitamboni Kova hakutuma taarifa hiyo.
ULINZI WAIMARISHWA HOSPITALINI
Hali ya ulinzi katika Hospitali ya TMJ iliimarishwa ndani na nje ya eneo hilo, kwa kuwapo kwa askari waliovalia nguo za kiraia.
Askari hao walionekana wakiimarisha doria nje ya wodi aliyolazwa Askofu huyo na kuzuia watu kusogelea wodi hiyo.
Nje
ya hospitali hiyo kulikuwapo na gari la Polisi lililokuwa limeegeshwa
likiwa na askari waliovalia nguo za kiraia, huku wengine wakiingia ndani
na kutoka kila mara.
Mbali na askari hao, pia walinzi wa Askofu Gwajima nao walionekana wakiwa karibu na wodi hiyo.
Ijumaa
iliyopita, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilimhoji
Askofu Gwajima kwa tuhuma za kumkashifu na kumtukana hadharani Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali
Pengo.
Muda
mfupi wakati wa mahojiano hayo yakiendelea, Askofu Gwajima alizimia
ghafla akiwa kwenye chumba cha mahojiano katika Kituo cha Polisi Kati.
Kufuatia
hali hiyo, Askofu huyo alipelekwa katika hospitali tofauti ikiwamo
ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na mwishowe kupelekwa TMJ
tiko
tiko
Post a Comment