tiko
tiko
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amekacha uzinduzi wa chama kipya cha ACT- Tanzania,
Taarifa
kutoka kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, Prof. Lipumba
amekacha kuhudhuria uzinduzi wa ACT kwa kile kilichoitwa, “hofu ya
kuchafuka.”
“Prof. Lipumba hakuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya mahusiano yake na Chadema, ambacho ni moja ya vyama vinavyounda UKAWA,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CUF.
Chama cha ACT, kinaundwa kwa asilimia kubwa na waliokuwa viongozi na wanachama kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Prof.
Lipumba alikuwa miongoni mwa wasomi wa ndani na nje ya nchi walioalikwa
kutoa mada katika uzinduzi wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es
Salaa, leo 29 Machi 2015.
Mbali
na Prof. Lipumba, wengine ambao wamekacha uzinduzi wa ACT-Tanzania, ni
Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa
kwanza wa Ghana, Osagyefo Kwame Nkrumah.
Katika
orodha hiyo, walitajwa kuwamo pia, Ababu Namwamba-Katibu Mkuu wa Chama
cha ODM cha Kenya; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
wa Jamhuri ya Kenya; mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini;
kiongozi wa vyama rafiki vya Ujerumani, Die Linke na Umoja wa vyama vya
mrengo wa kushoto Progressive Alliance.
Wachambuzi
wa mambo ya kisiasa wanasema, hatua ya Prof. Lipumba kutohudhuria
uzinduzi wa mkutano huo, unaashiria kutokubaliana na uadilifu wa
waanzilishi wa ACT.
Aidha, hatua ya Prof. Lipumba kususia uzinduzi wa ACT, yaweza kuwa imesukumwa na kutaka kuimarisha umoja ndani ya UKAWA.
ACT
kimezindua ilani yake ya uchaguzi, kutangaza viongozi; na kudai kuwa
kitarejesha Azimio la Arusha, ambalo lilikufa kabla ya muasisi wake,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa bado yuko ulimwenguni.
tiko
tiko
Post a Comment