Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

ALA PASAKA KWA KICHAPO AKIDAIWA KUWA MWIZI!

Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Anton, Jumapili ya Pasaka alikula sikukuu kwa kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kwa madai kuwa ni kibaka.Tukio hilo lililotokea saa 12 asubuhi maeneo ya Sinza Afrikasana ambapo walioshuhudia tukio hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa, kijana huyo aliyefahamika mtaani hapo kama muokota chupa, ilidaiwa kuwa  alikurupushwa kutoka katika nyumba moja ambako alienda kwa gia ya kuokota chupa, akataka kukwapua kitu.


 Anton akivuja damu baada ya kupewa kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kwa kosa la wizi.
 “Baada ya kukurupushwa katika nyumba hiyo, kijana huyo alitoka mkuku mpaka katika nyumba moja ambako alimkuta dada mmoja akifagia na kuingia ndani ya geti  kisha kujifungia,” alisema shuhuda mmoja.

Baada ya muda wakatokea watu waliomkurupusha ndipo dada huyo akawaambia kuwa mtuhumiwa wao ameingia ndani baada kulikuta geti hilo wazi wakati akifanya usafi na alikuwa amejifungia kwa ndani.
Habari hiyo iliwafanya baadhi ya vijana kudandia geti ili kuingia ndani, hata hivyo, kijana huyo alipoona watu hao wakiruka getini naye akaruka ukuta upande wa pili na kukimbia.Akipakizwa kwenye gari safari kuelekea kituoni.
 Lakini juhudi zake hizo za kutaka kutoroka hazikuzaa matunda kwani alidakwa hatua chache kutoka kwenye ukuta wa ua wa nyumba hiyo na kuanza kula kichapo kikali ambacho kilisababisha kuchanwa kichwani na damu nyingi ‘kumwagika.’
 Kijana huyo aliokolewa na askari polisi waliokuwa doria wakiongozwa na Kamanda Rashidi wa Kituo cha Polisi Mabatini waliokuwa katika gari yao ya doria.

Moja ya jeraha kubwa alolipata kichwani baada ya kichapo.
Kamanda huyo na askari wenzake walifanya kazi kubwa kuzuia raia wasilete madhara zaidi kwa kijana huyo huku wakiwaambia wananchi kuwa siyo busara kujichukulia sheria mkononi, walimkamata wakampeleka kituoni kwa hatua zaidi.

Hali tete jijini dar..!! Polisi Yazuia Wafuasi Wa Askofu Gwajima.....Vikosi vya Mbwa, Farasi,Magari sasa kila Kona.


Jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  limesema  wafuasi  wa  Askofu  mkuu  wa  kanisa  la  ufufuo  na  uzima,Josephat  Gwajima  wasithubutu  kutia  mguu  eneo  atakalohojiwa  askofu  huyo.

Kauli  ya  jeshi  hilo  imekuja  siku  chache  baada  ya  Askofu  Gwajima  kuwataka  wafuasi  wake  kumsindikiza  leo  kituo  cha  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  ambako  anahitajika  ili  kuhojiwa.

 Msimamo huo  ulitolewa  jana  na  kamishna  wa  polisi  katika  kanda  hiyo, Suleiman  Kova  wakati  akizungumza  na  mtandao  huu  ambapo  alisisitiza  kuwa  anayehitajika  kufika  katika  kituo  hicho  ni  Gwajima  na  mwanasheria  wake.

Kamishna  Kova  alisema  ni  vema  wafuasi  hao  wakaendelea  na  kazi  zao  za  uzalishaji,kwani  kwenda  kituoni  hapo  bila  mwito  au  kukamatwa  ni  kosa.

Kova  alisema  eneo  hilo  haliruhusiwi  watu  kukusanyika, hivyo  kwa  usalama  wao ni  vyema  wakaendelea  na  shughuli  zao  na  kuliacha  jeshi  hilo  lifanye  mahojiano  na  Askofu huyo  wakiwa  huru.

"Napenda  kutumia  nafuasi  hii  kumuomba  Gwajima  awaambie  wafuasi  wake  hawahitajiki  kufika  eneo  hilo  kwani  anayehitajika  ni  yeye  na  mwanasheria  wake," alisema  Kova.

Kova  alisema  iwapo  kila  mtu  atafuata  taratibu  hakuna  nguvu  itakayotumika  kutoka  jeshi  la  polisi, lakini  endapo  watakiuka  hakuna  njia  mbadala  ambayo  inaweza  kutumika  zaidi  ya  kutumia  nguvu.

Kauli  ya  Kova  inakuja   kutokana  na  kauli  ya  Gwajima  aliyoitoa  wakati  wa  sikukuu  ya  pasaka  kuwataka  wafuasi  wake  kujitokeza  katika  kituo  hicho  wakati  atakapokwenda  kuhojiwa.

Gwajima  alisema  lengo  la  kuwataka  wafuasi  hao  kujitokeza  ni  ili  waweze  kujua  kila  kitu  kinachoendelea  katika  sakata  hilo  kwani  kuna  taarifa  ambazo  zimekuwa  zikizushwa  na  watu  kupitia  mitandao  mbalimbali.

Akizungumzia  hali  ya  usalama  katika  jiji  la  Dar, Kova  alisema  ni  shwari  na  kuahidi  kuwa  wanaendelea  na  oparesheni  ya  kukamata  wauza  dawa  za  kulevya, wahalifu  na  kulinda  maeneo  ya  fukwe.

Pia, alisema  wamejipanga  kukabiliana  na  vitendo  vya  kigaidi  ambapo  wanafanya  uchunguzi  kila  mahali  kwa  kutumia  vikosi  vya  mbwa, farasi,helkopta, magari, pikipiki  na  kutembea  kwa  miguu  katika  maeneo  yote  ya  jiji.

AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUGUNDULIKA KUHUSIKA NA KIFO CHA MAREHEM

Picha  Ya  Maktaba

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
 
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
 
Diwani wa Kata hiyo amesema alipata taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote kukimbiwa baada ya tukio hilo.
 
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.

Yemen:Houthi yavamia mji wa Aden

Wapiganaji Yemen wanakamia Aden
Wapiganaji waasi nchini Yemen wamezidisha mapigano yao katika hatua za kuuthibiti kabisa mji wa Aden.
Nyumba kadhaa zimechomwa moto huku sauti zikisikika kutoka kwenye vipaza sauti misikitini,
ya kuwataka raia wote wa mji huo kujitokeza ili kutetea mji wao usitwaliwe na waasi.
Wakati huo huo, kuna ripoti kuwaege za muungano zikiongozwa na majeshi ya Saudi Arabia zinazounga mkono
Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano
serikali ya Yemen, yakirusha mabomu katika ngome ya waasi katika viunga vya mji wa Aden upande wa kazkazini.
Awali Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano, yanayoongozwa na Saudi Arabia,
katika makabiliano dhidi ya kundi la waasi wa Kishia la Houthi, nchini Yemen.
Awali hali ya taharuki ilitanda kote katika mji huo wa pwani baada ya
Iran imezua taharuki baada ya kutuma Manuari yake katika bahari ya Yemen
Iran Kutuma manuari mbili za kivita katika bahari inayopakana na eneo la Aden nchini Yemen.
Kamanda mmoja wa jeshi la Iran amesema manuwari hizo zimetumwa katika eneo hilo kulinda taifa lake kutokana na uharamia.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa hatua hiyo huenda ikachochea uhasama zaidi katika eneo hilo.
Saudi Arabia inaongoza jeshi la muungano linalokabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa kishia nchini Yemen, wapiganaji ambao wanakisiwa kupewa misaada na utawala wa Tehran.

Bei za vyakula zapaa, mfumuko wa bei mwezi Machi wafikia asilimia 4.2

Bidhaa za vyakula katika moja ya masoko nchini. Picha ya mtandao. 
Upungufu  wa chakula kwa baadhi ya mikoa nchini umeendelea kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei wa Taifa kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula zimeongezeka.
“Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapimwa kwa kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi,”alisema.
Aliongeza: “Hivyo kutokana na ongezeko la bei za bidhaa hizo pamoja na huduma zote kwa kaya zimesababisha mfumuko wa bei wa taifa,”alisema Kwesigabo.
Aliendelea kueleza kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa hizo zimesababisha mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi iliyopita kuongezeka hadi ukufikia asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 ya mwezi Februari mwaka huu.
Kwesigabo alisema, ongezeko la mfumuko wa bei kwa mwezi Machi umesababishwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Machi mwaka huu tofauti na ilivyokuwa kwa Machi mwaka jana.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wataendelea kushuhudia bei za vyakula zikiendelea kupanda na kwamba bei waliyokuwa wakinunua bidhaa za vyakula hapo awali itabadilika.
Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi uliopita ikilinganishwa na mwezi Septemba, 2010 alisema, uwezo wa Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 64 na senti 15 mwezi Machi mwaka huu kutoka Septemba, 2010.
“…ikilinganishwa na Sh 64 na senti 59 ilivyokuwa Febriari mwaka huu,”alisema Kwesigabo.

ICC: IS imetenda makosa ya jinai

Kiongozi wa Mashtaka wa ICC amesema kuwa ISIS imetekeleza uhalifu wa hali na ukatili mkubwa nchini Syria na Iraq
Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, iliyoko the Hague Uholanzi, Fatou Bensouda, amesema kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State,
limetekeleza uhalifu wa hali na ukatili mkubwa nchini Syria na Iraq.
Bensouda amesema uhalifu huo unahatarisha amani, usalama sio wa eneo hilo tu bali dunia kwa ujumla, lakini amekariri kuwa Iraq na Syria sio wanachama wa mahakama hiyo.
Maelfu ya wapiganaji wa kigeni wamejiunga na wapiganaji wa ISIS
Wengi wa wapiganaji wa kundi hilo ni raia wa Kigeni ndio maana mwendesha mashtaka huyo mkuu anasema hana budi ila kusalimu amri.
Maelfu ya wapiganaji wa kigeni wamejiunga na wapiganaji wa ISIS, wakiwemo raia wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji, Australia na Tunisia.
Licha ya kuwa nchi hizi ni wanachama wa mahakama ya ICC, Bensouda anasema kuwa kundi hilo la ISIS linaongozwa na raia wa Iraq na Syria.
Na kwa sababu nchi hizo sio wanachama wa ICC, Bi Bensouda amesema kuwa uwezekano wa kuchunguza wale waliohusika zaidi chini ya uongoza wa ICC ni finyu kabisa.
Kiongozi wa Mashtaka wa ICC amesema kuwa ISIS imetekeleza uhalifu wa hali na ukatili mkubwa nchini Syria na Iraq
Aidha ametoa wito kwa mataifa wanachama kutafuta mbinu za kuwawajibisha wale waliohusika.
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa halina mamlaka kuwasilisha kesi katika mahakama hiyo kuhusiana na hali ilivyo nchini Iraq na Syria.
Ameongeza kuwa kuwa uhalifu unaondelea kutekelezwa nchi humo unakiuka maadili yote ya kibinadam na ni sharti waliohusika kufunguliwa mashtaka

Wasomali walalama kufungwa kwa Hawala Kenya

Kenya imefunga mashirika 13 na akaunti 86 za watu wanaodhaniwa kufadhili Al Shabaab
Jamii ya wasomali nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali nchini humo kufunga mashirika kumi na tatu ya ubadilishaji wa sarafu za kigeni na usafirishaji pesa maarufu kama Hawala.
Malalamishi yao ni kuwa hatua hiyo itasababisha matatizo makubwa kwa wasomali ambao daima wanategemea njia hiyo, kuwatumia jamaa zao fedha kutoka mataifa ya kigeni.
Hatua hiyo imefanyika baada ya shambulio la Al-Shaabab katika Chuo kikuu mjini Garrisa juma lililopita.
Serikali ya Uhuru Kenyatta inasema kuwa ni mojawepo ya njia ya kuzuia al-Shabaab kupata fedha ili kupanga na kutekeleza mashambulio zaidi.
Hali ya hatari ya kutotembea nje usiku pia imewekwa katika majimbo yaliyo na wasomali wengi kazkazini mashariki mwa Kenya.
Akaunti za Benki za watu themanini na sita zinazodhaniwa kufadhili ugaidi pia zimesitisha.
Wasomali walalama kufungwa kwa Hawala Kenya
Gavana wa benki mkuu ya Somalia Bashir Issa Ali ameiambia shirika la habari la Reuters amethibitisha kuwa amepokea ilani hiyo kutoka kwa benki kuu ya Kenya.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Kenya Amina Mohamed amesema kuwa nchi yake imeomba msaada wa kijasusi kutoka mataifa ya magharibi
kufuatia shambulizi baya zaidi katika miaka ya hivi punde iliyosababisha vifo vya watu 148 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa.
-bbc

Wanafunzi wa sekondari kibondo walalamikia ukosefu wa walimu wa sayansi.

Wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya ya kibondo mkoani kigoma wamelalamikia ukosefu wa walimu wa sayansi katika shule zao licha ya kasi kubwa ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.
Wakizungumzia changamoto hiyo, wanafunzi katika shule ya sekondari Biturana wamesema shule nyingi zina mwalimu mmoja huku baadhi ya shule wanafunzi wakiwa hawasomi masomo ya sayansi kutokana na ukosefu wa walimu,ambapo wameitaka serikali kuhakikisha walimu wa sayansi wanapatikana ili wanafunzi waweze kusoma nadharia na vitendo.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo Hassana Masala amesema wilaya hiyo imefikia zaidi ya asilimia themanini ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule zake huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya kibondo  Fred Eliasafu amesema wilaya hiyo inaendelea na ujenzi wa nyumba za walimu katika shule zake ili kuhakikisha walimu wanaopangwa wanapata mahali pa kuishi.

TANESCO Comes New luku Facing Problem Now


Electric utility in (TANESCO) hopes to change the system of care Electricity Pay As Utumiavyo (Maluku) and paste it to relieve discomfort modern customers.

Indicated that the system used now is a problem due to these changes, the new system may put into force next month. That was made yesterday by Tanesco Relations Manager, Adrian Severin.
He said the system will be decided upon, will be modernized and that will help users quickly find the services of Maluku. He said it is a computer system, modern and fast, you kaotibu nuisance they are getting users to access the Maluku.
'' The system you may be able to serve more customers and quickly within three seconds, compared to the old system which had been used more than a minute or 30 seconds, '' said Severin.
Added the preparation of such a system, have been completed and that will be using cellphones and agents who sell Maluku, will continue to provide the service.
'' Agents MaxMalipo and all calls are delivered as Tigo, Airtel, Zantel and Vodacom will continue to provide this service, but it will be fast and that there will be no trouble networks, '' he said.
Referring to the issue of lack of access to services of Maluku since yesterday evening, Severin said the service was not available, due to a network problem.
'' Sometimes cellphones do not have the problem of networks, but you find them is under Tanesco networks, so that Tanesco becomes available similar to the network, but the number zinasumbua, '' said Severin.
He stressed that in order to be found quickly to the care of Maluku, Tanesco and all calls will be required to provide such services and networks to be equal. However, he said the service is available at the moment.
For a long time, the users of the services of Maluku, have complained about the poor quality of care, amounting to make its customers fail to have electricity for several days, due to structural problems in mechanical services Maluku.

Mgomo wa madereva nchi nzima wanukia

Drivers various fire agencies, they intend to share a nationwide strike Friday this week, pressuring the government to remove various impediments facing unemployment, including guaranteed with the mandate of wanting to read.
Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bw. Rashid Saleh, Madereva hao wameiambia East Africa Radio kuwa suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali.
Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.
Saleh ametaja madereva wanaounda muungano huo kuwa ni wa bodaboda, bajaj, teksi, daladala, mabasi ya safari fupi, mabasi ya safari ndefu na za nje ya nchi pamoja na madereva wa magari yote ya mizigo.
According to the leader of the drivers union, meeting on Friday will be the only limiting factor if these drivers bark or continue to work because they are tired of contempt even for basic things that affect their lives.
Some of the contempt he mentions include owners of buses (ie their employers) to call them are criminals while an adult, with a family, working lawful and requiring respected.

Kakobe Amshukia Lowassa...Awataka Watanzania Kususia Kura Ya Maoni Maana Katiba hiyo ni ya Kishetani na Mwandishi Wake Ni "Nyoka Wa Makengeza" (Shetani)

Akihubiri siku ya Pasaka katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo Mwenge katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe alisema kwamba, inajulikana wazi kwamba Lowassa amekuwa anautaka Urais kwa udi na uvumba kwa miaka mingi, hata mwaka 1995 alijitosa hadharani kuuwania, sasa anapodai kwamba hivi sasa kuna makundi yanayokwenda kwake kumshawishi agombee Urais, kana kwamba yeye hataki Urais, anakuwa anamdanganya nani?

Although in this sermon two hours, Kakobe did not mention Lowassa by name, however Kakobe said, "There are other people who have known clearly that they have been urging the president to incense and incense, for many years, but now they say there are groups of people yanawafuata home, convince the Presidential candidates, as they wish Presidency, so these people who lied?

Ingawa katika mahubiri hayo ya saa mbili, Kakobe hakumtaja Lowassa kwa jina, hata hivyo Kakobe alisema, "Wako watu wengine ambao inajulikana wazi kwamba wamekuwa wakiutaka Urais kwa udi na uvumba, kwa miaka mingi, lakini hivi sasa wanasema kuna makundi ya watu yanawafuata nyumbani, kuwashawishi kugombea Urais; kama vile hawautaki Urais, hivi watu hawa wanamdanganya nani?
 
"Na wale wanaokwenda kumshawishi mtu ambaye kwa miaka mingi, anajulikana kwamba anautaka Urais, hawajui kwamba nao wanafanywa kuwa wajinga? Mtu anayejulikana kwa muda mrefu kwamba anautaka Urais, ni vema akatangaza tu moja kwa moja nia yake, bila haja ya ghiliba."

Katika mahubiri yake yenye kichwa, "UPOTOSHAJI WA UKWELI", Kakobe alieleza jinsi Gavana wa Kirumi, au liwali Pontio Pilato, alivyojiunga na Viongozi wengine kupotosha ukweli wa kufufuka kwa Yesu, na kusema kwamba wanafunzi wake waliuiba mwili wake, wakati askari walinzi walipokuwa wamelala, na kuwadanganya watu, ingawa wao wenyewe waliujua ukweli.
 
"Pilato aliwadanganya watu hao kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli ulikuwa dhahiri, walipomwona Yesu kati yao kwa muda wa siku 40. Unaweza kuwadanganya watu kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli hudhihirika, na kumfedhehesha yule aliyeupotosha ukweli huo", alisema.

Aliendelea kusema kuwa, hata leo kuna upotoshaji wa kweli mbalimbali za kiroho na kimwili. Baada ya kuelezea juu ya baadhi ya kweli za kiroho zilizopotoshwa, aliwageukia wanasiasa waongo, akianza kwa kutoa mfano wa Waziri wa Habari wa Iraq, wakati wa vita ya mwaka 2003, Muhammad Saeed al-Sahhaf, aliyekuwa akipotosha ukweli kuhusu jinsi Iraq ilivyokuwa inapigwa vibaya katika vita hivyo, na akaendelea kusema;
 
"Kabla sijaendelea, nifafanue kwanza juu ya watu wanaopotosha ukweli, kwa kusema kwamba eti Wachungaji hawapaswi kuwakemea wanasiasa wananapopotoka. Watu hawa hawajui Biblia. Katika MAMBO YA WALAWI 4:22-23, Biblia inasema, Mtawala akifanya dhambi, inampasa Kuhani yaani Mchungaji, kumjulisha dhambi yake."

Kakobe aliendelea kusema kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo Watanzania wawe makini na wanasiasa waongo wanaofanya uongo kuwa sehemu ya siasa zao.
 
"Siasa, ni Sayansi, inaitwa POLITICAL SCIENCE, na "any kind of science only deals with facts". Wanasiasa hawana budi kuwa wakweli kwa kuwa siasa ni sayansi.
 
"Siasa siyo mchezo mchafu, bali baadhi ya wanasiasa ndiyo wachafu. Msidanganywe tena na wanasiasa ambao watakuja kwenu mwaka huu na ahadi za uongo za kuibadili miji na kuifanya kuwa kama New York, kwa miaka mitano; na wengine hawana AIBU, wanaweza hata kuwaambia wakazi wa Dodoma kwamba watawaletea meli! Hamna budi kuyachunguza kwa makini maneno yao, na kuona kama ni ya kweli."

Kuhusu Katiba, Kakobe aliwaunga mkono Maaskofu waliowapa Wakristo maelekezo ya kuikataa Katiba Pendekezwa, katika Kura ya Maoni, na kusema kwamba hiyo ndiyo kazi ya Mchungaji.
 
"Mchungaji, pia ni Mwalimu, kazi yake ni kuchunga na pia kulisha kondoo (YOHANA 21:15-17), na Biblia inafafanua juu ya kazi ya Mwalimu katika ISAYA 30:20-21, ikieleza kwamba Mwalimu anatakiwa kuwaambia anaowaongoza, "Njia ni hii ifuateni, wageukapo kwenda kulia au kushoto".
 
Aliendelea kusema, "Kumekuwa na udanganyifu au upotoshaji wa ukweli kuhusu Katiba, tangu katika hatua za mwanzo kabisa za mchakato wa Katiba, ambapo Chama kimoja cha siasa, kiliwapachika makada wake katika vikundi mbalimbali, ili kiwe na wajumbe wengi.
 
"Kwa mfano Kingunge Ngombale Mwiru aliwawakilisha waganga wa kienyeji, lakini cha ajabu, ukienda kwake hata leo, hakuna kibao kwake kinachozitambulisha kazi zake za uganga wa kienyeji, kama ilivyo kwa waganga wengine! Siyo hilo tu, kote duniani, Katiba yoyote ya nchi, lazima itokane na muafaka wa Kitaifa, ili Katiba hiyo iwe na sifa ya kusomeka katika Utangulizi wake, "SISI WANANCHI".
 
"Hapa kwetu, watawala hawakutaka kabisa muafaka katika kutengeneza Katiba yetu, lakini wanadai eti, Katiba Pendekezwa, ni bora kuliko zote Afrika! Huu ni upotoshaji wa ukweli, wa hali ya juu sana."

Aliendelea kusema kwamba, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Kura ya Maoni, hazikuzingatiwa kikamilifu katika mchakato huo uliojaa udanganyifu. 
 
"Sheria ya Kura ya Maoni, Ibara ya 5(3), inasema kwamba kungetakiwa kuwepo na elimu kwa wapiga kura, kwa siku 60, mara tu baada ya Tangazo la Katiba Pendekezwa katika Gazeti la Serikali Na. 382 lililotolewa tarehe 10.10.2014, lakini elimu hiyo iliyopaswa kutolewa na Tume ya Uchaguzi, haijafanyika hadi hivi leo! 
 
V"ilevile, Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 4(3) na 4(4), inasema kwamba kungetakiwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali, SWALI LA KURA YA MAONI, ambalo wananchi wangelijibu kwa jibu la NDIYO au HAPANA, na pia Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 12(1) na 12(2) na Ibara ya 16(1) inasema kwamba, kungetakiwa kuwepo na Kamati mbili za Kura ya Maoni, Kamati moja ya NDIYO, na nyingine ya HAPANA, ambazo zingejumuisha wananchi wenye misimamo tofauti kutoka katika makundi mbalimbali katika jamii, na Kamati hizo zingepiga kampeni kwa siku 30. 
 
"Yote haya hayakuzingatiwa, lakini kinyume chake, Watawala hadi hivi leo, hawataki hata kusikia watu wakisema HAPANA kwa Kura ya Maoni, na wakati huohuo, wengine bado wanataka Kura ya Maoni ifanyike Aprili 30, pamoja na kwamba imetangazwa na Tume ya Uchaguzi, kwamba imeahirishwa!

"Wachungaji wengine wenye njaa, wanathubutu kusema kwamba eti kwa sababu kwenye Katiba Pendekezwa kuna Uhuru wa kuabudu, basi sisi Wachungaji tukae kimya, mengine hayatuhusu, hawa wana njaa kali, na upeo mdogo wa uelewa wa mambo haya.
 
"Mimi sina njaa, na ninasema kwa msisitizo, Katiba ni zaidi ya Uhuru wa kuabudu. Ilikuwa rahisi kwa Pilato kuwadanganya watu wa nyakati hizo, lakini leo ni kazi sana kuwadanganya watu wanaopata maarifa na habari juu ya yote yanayofanyika kote duniani, kwa TV, Redio, Magazeti, Intaneti na Mitandao ya kijamii. 
 
"Watu wanajua kwamba kote ulimwenguni, Katiba ya Wananchi hutokana na muafaka, na Kura ya Maoni, hufanyika baada ya Kampeni ya NDIYO na HAPANA, kama ilivyofanyika Kenya ambako waliosema NDIYO waliitwa kundi la NDIZI, na waliosema HAPANA waliitwa kundi la CHUNGWA.
 
"Waliowaambia Wakristo wapige kura ya HAPANA kwenye Kura ya Maoni, ninawapa asilimia 90, hata hivyo kwa unyenyekevu, mimi ninaomba kuhitilafiana nao, kwa kuongeza kwamba Kura ya Maoni inapaswa kususiwa kabisa, kwa sababu kushiriki katika Kura hiyo, ni kuuhalalisha udanganyifu wa Watawala hawa, na kujifedhehesha mwishoni.
 
"Tangu mwanzo, watu hawa walitumia ubabe na wizi wa kura wa dhahiri katika Bunge la Katiba, na kutangaza kura feki za NDIYO za mahujaji na wajumbe wengine ambao hawakuwepo ukumbini wakati wa kupiga kura, na pia kura za Wazanzibari feki, na hivyo kupitisha kwa lazima, Katiba Pendekezwa. 
 
"Wamedhamiria kufanya hivyohivyo hata katika Kura ya Maoni, ili kuipitisha kwa lazima Katiba yao Pendekezwa; ukizingatia kwamba, ili kutimiza kusudi hilo, wameweka sheria mbaya kwa makusudi ya kuhalalisha udanganyifu.
 
"Kwa mfano Sheria ya Kura ya Maoni Ibara ya 34(2), inahalalisha wapiga kura walioandikishwa Tanzania Bara, kwenda kupiga kupiga Kura ya Maoni, huko Zanzibar. Katika mazingira haya, Kura za HAPANA zitasaidia nini? Ni kuhalalisha tu udanganyifu wao, na kujifedhehesha.

"Mwandishi Mkuu wa Katiba Pendekezwa, yeye mwenyewe amesema anapenda aitwe JOKA LA MAKENGEZA! Niliposikia juu ya Jina lake hili, nilipigwa na butwaa! 
 
Katika Biblia, Joka ni Ibilisi au Shetani (UFUNUO 12:7-9; 20:1-2), maana yake ni kwamba Mwandishi Mkuu wa Katiba Pendekezwa, ni Joka yaani Shetani, na hivyo tunaweza kusema Katiba hiyo ni ya Kishetani, maana imetokana na Shetani ambaye ni Joka lililoko kuzimu! 
 
"Kumbe basi, siyo tu kwamba Katiba Pendekezwa imeahirishwa, ila ni kwamba Mungu ameikataa tangu siku ya kwanza ya mchakato wake!
 
"Kwa sasa tuwaze tu kujiandikisha kwa wingi katika Uandikishaji wa Wapiga Kura, kwa BVR, na kuwa tayari tu kwa Uchaguzi Mkuu, na kuisahau kabisa Kura ya Maoni."

SOURCE: Lead Story Tanzania Daima 7.4.15; na CD ya Neno la Pasaka la Kakobe

Vigogo Chadema Handeni wasimamishwa uongozi....Chadema trunks Handeni not made to stand management

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Governing Council of the Party for Democracy and Development (Chadema) Tanga Region, leading limewasimamisha Chairman, Secretary and members of the party Handeni District for allegedly failing to take responsibility within the party as well.
 
Likewise, the council has taken action similar to that party secretary of Muheza district.
 
Baraza la Uongozi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Tanga, limewasimamisha uongozi Mwenyekiti, Katibu na wajumbe wa chama hicho Wilaya ya Handeni kwa madai ya kushindwa kuwajibika ndani ya chama pamoja.
 
Kadhalika, baraza hilo limechukua hatua kama hiyo kwa katibu wa chama hicho wilayani Muheza.
 
Akielezea hatua hiyo, Katibu wa Chadema mkoani Tanga, Ismail Masoud, alisema uongozi wa chama hicho umewasimamisha kazi viongozi hao hadi uchunguzi dhidi yao utakapomalizika.
 
Aliwataja viongozi hao kuwa ni Jadi Bamba, ambaye ni Mwenyekiti, Ibrahim Ramia (Katibu) pamoja na wajumbe sita wa Baraza la Uongozi.
 
Alisema viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kushindwa kukisaidia Chama kunyakua nafasi za uenyekitiwa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni na kuunda makundi ndani ya chama hicho.
 
“Baraza la Uongozi Chadema Mkoa, limepitisha uamuzi mmoja wa kuwasimamisha kazi Mwenyekiti, Katibu na wajumbe wote wa wilaya kwa tuhuma za kukihujumu Chama,” alisisitiza.
 
Alifafanua kuwa viongozi hao wamesimamishwa hadi uchuguzi dhidi ya tuhuma zao utakapokamilika.
 
Masoud alisema kutowajibika kwa makatibu kumesababisha kutoa mwanya kwa vyama pinzani kujiimarisha na kuchukua maeneo ambayo tayari yalikuwa na ushawishi mkubwa wa Chadema na kuwa na uhakika katika uchaguzi mkuu ujao kufanya vizuri nafasi za udiwani.

Ndesamburo kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu wauaji..,,Ndesamburo submit a motion in parliament about the killers

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo

Member of the Board of Trustees of the Association for Democracy and Development (Chadema) and Member of Moshi, Philemon Ndesamburo, has planned to submit a motion in parliament, he urged the Ministry of Interior of the State, provide information about police failure to arrest four suspects of murder the intent of the former manager of a popular pub in here, James John.

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amepanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni, akiitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoa maelezo kuhusu Jeshi la Polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa meneja wa baa moja maarufu mjini hapa, James John.
 
James aliuawa Juni 06, mwaka 2009 na watu wanne wanaodaiwa kuwa ndugu wa familia moja, huko katika Kijiji cha Kindi-Kibosho, Wilaya ya Moshi. 
 
Jana, Ndesamburo alisema katika hoja yake atamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, kulieleza Bunge sababu zinazolifanya Jeshi la Polisi kushikwa na kigugumizi cha kuwakamata watuhumiwa hao na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
 
“Katika maelezo ya hoja hiyo, nitataka pia serikali kueleza lilipo jalada la uchunguzi wa mauaji hayo. Nimeamua kuchukua uamuzi huu, kwa kutumia Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo imelipa Bunge, Mamlaka ya kuishauri na kuisimamia Serikali na vyombo vyake katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Ndesamburo.
 
Alisema yeye kama Mbunge wa Moshi Mjini, ambaye amekuwa akiheshimu utawala wa sheria, ameamua kulichukua jambo hilo na atalipeleka bungeni baadaye mwezi huu ili kulisukuma Jeshi la Polisi liwajibike kutekeleza wajibu wake.
 
Jeshi la Polisi liliwakamata na kuwafungulia mashtaka ya mauaji, watu wawili tofauti (Majina yao yamehifadhiwa), ambao hata hivyo, waliachiwa huru na Mahakama baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), kudai hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa hao.
 
Wakati, Ndesamburo akijitwisha msalaba huo, baadhi ya ndugu wa marehemu James wamemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, kuingilia kati sakata hilo ili kutoa msukumo utakaopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo.

WASTARA AKATA MAUNO HADHARANI USIKU WA PASAKA

Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akicheza kwa hisia.

WONDERFUL! Staa film brain, Stara Juma eve of Monday wrote a history of its kind within the National Stadium Entertainment Dar Live prevailing Mbagala-Zakhem, Dar drawing shows the power stage so make fans tablet attendees hall when a trance they believe as is he.

AJABU! Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma usiku wa kuamkia Jumatatu aliandika historia Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, Dar kwa kuonesha shoo ya nguvu jukwaani hivyo kuwafanya mashabiki kibao waliohudhuria ukumbini hapo kupigwa butwaa wasiamini kama ni yeye.


Katika shoo hiyo ya Sikukuu ya Pasaka iliyotambulika kwa jina la Mwana Dar Live, wasanii, Msaga Sumu, Ali Kiba na Isha Mashauzi walitumbuiza, lakini Wastara alihudhuria maalum kwa ajili ya  Ali Kiba.
ATINGA NA TIMU KIBA
Wakati jukwaani akiimba msanii wa muziki wa Vigodoro, Msaga Sumu, kundi kubwa lililojulikana kama ‘Team Kiba’ likiwa na watu zaidi ya kumi lilitinga ukumbini hapo likiongozwa na Ali Kiba mwenyewe huku Wastara akiwa miongoni mwao.
AJIWEKA KARIBU NA DADA KIBA
Katika hali ya kushangaza, punde baada ya kundi hilo kutinga ukumbini hapo, Ali Kiba alipanda jukwaani na kumuacha Wastara akiwa sanjari na dada wa Kiba aitwaye Zabibu Kiba huku muda wote akionekana kucheka na kurusha mikono kwa shangwe.

astara Juma akichekecha na kucheketua.

Kudhihirisha kuwa amekuja kama Team Kiba, staa huyo alionekana kukongwa na nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na Kiba kiasi cha kuanza kuserebuka hadharani huku Zabibu akimpa sapoti kwa kuibiaibia kiaina.

Kitendo cha kuendelea kuserebuka nyuma ya jukwaa kiliwashangaza baadhi ya watu huku wengine wakiwa hawaamini kama ni Wastara wanayemjua wao.
“Jamani kweli huyu ni Wastara tunayemjua au? Mh! Mimi sijawahi kumwona akisakata muziki kama hivi. Ama kweli Dar Live ndiyo kiwanja cha burudani, ingekuwa viwanja vingine sidhani kama angejiachia,” ilisikika sauti ya shabiki mmoja wa muziki baada ya kukosa uzalendo kwa kumuangalia Wastara.
WATU WAPIGWA BUTWAA
Baada ya kusakata mauno nyuma ya jukwaa kumnogea na kusababisha kuzua minong’ono ya hapa na pale, mdada mmoja alionekana kuvutiwa na staa huyo na kuamua kumshika mkono kwa kumtaka apande jukwaani ili akawadhihirishie mashabiki wote kuwa, anayaweza kama si kuyamudu!

Akizidi kudatisha mashabiki.
Awali, Wastara alionekana kukataa katakata na kugeuza kichwa huku na kule kwa aibu lakini dakika kama tatu mbele, ghafla aliibukia jukwaani ambapo Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba walikuwa wakiimba pamoja wimbo wa Chekecha Cheketua na kuwafanya mashabiki kupigwa butwaa.
ATUMIA ZAIDI YA DAKIKA TATU
Wastara aliyevaa suruali nyesi na juu kitop cha jinzi, akiwa jukwaani hapo, bila kupepesa macho alianza kwa kuwanyooshea mkono mashabiki wake kisha akawageuzia mgongo na kuanza kuyakata mauno kwa staili ya Chekecha Cheketua huku baadhi ya mashabiki hao wakiwa hawaamini kwa kile alichokuwa akikifanya, wengine walitamani kupanda jukwani wakajirushe naye.

Pale jukwaani, Wastara alitumia zaidi ya dakika tatu kiasi cha kuwafanya Ali na Abdu kushusha vipaza sauti vyao na kumuangalia staa huyo akiwafundisha mashabiki staili ya wimbo huo wa Cheketua.
Hadi anaondoka kwenye jukwaa hilo la kisasa, mashabiki walikuwa wakimshangilia staa huyo wengine wakisema kumbe ni fundi wa kucheketua!
“Loo! Wastara bwana! Leo amenifanya nimpende zaidi, kumbe anayaweza, huwezi amini kabisa. Ama kweli Mungu kila mtu kampa kipawa chake,” alisema shabiki mmoja huku macho yake yakimsindikiza Wastara wakati anaondoka.
TUJIKUMBUSHE
Wastara alifunga ndoa Juni 6. 2009 na msanii mwenzake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ (sasa marehemu). Wakiwa wachumba wawili hao walipata ajali mbaya ya bodaboda maeneo ya Tabata jijini Dar ambapo Wastara alivunjika mguu na baadaye kukatwa kabisa hivyo kumfanya awekewe mguu wa bandia.
Katika kipindi chote hicho na hasa baada ya kifo cha Sajuki, Wastara amekuwa akiishi katika mazingira ya kidini na hakuwahi kuonekana akicheza muziki hadharani kama vile, hivyo alichokifanya usiku huo kwake ni kuandika historia mpya ya maisha yake ya ustaa.
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top