Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Wanafunzi wa sekondari kibondo walalamikia ukosefu wa walimu wa sayansi.

tiko tiko
Wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya ya kibondo mkoani kigoma wamelalamikia ukosefu wa walimu wa sayansi katika shule zao licha ya kasi kubwa ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.
Wakizungumzia changamoto hiyo, wanafunzi katika shule ya sekondari Biturana wamesema shule nyingi zina mwalimu mmoja huku baadhi ya shule wanafunzi wakiwa hawasomi masomo ya sayansi kutokana na ukosefu wa walimu,ambapo wameitaka serikali kuhakikisha walimu wa sayansi wanapatikana ili wanafunzi waweze kusoma nadharia na vitendo.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo Hassana Masala amesema wilaya hiyo imefikia zaidi ya asilimia themanini ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule zake huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya kibondo  Fred Eliasafu amesema wilaya hiyo inaendelea na ujenzi wa nyumba za walimu katika shule zake ili kuhakikisha walimu wanaopangwa wanapata mahali pa kuishi.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top