tiko
tiko
Mbunge
wa ludewa Mhe.Deo Filikunjombe amesema elimu zaidi inahitajika
kuwaunganisha watanzania kuondoa mpasuko uliojitokeza wakati wa mchakato
wa katiba mpya na mapendekezo ya muswaada wa sheria ya kuridhia
kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi hapa nchini.
Mheshimiwa
Filikunjombe ametoa ushauri huo katika salamu zake za pasaka
alipohudhuria ibada ya sikukuu ya pasaka katika kanisa la Aglikana na
kanisa katoliki parokia ya mavanga wilayani ludewa.
Amesema
kabla ya kufikia uamuzi wa kupitisha katiba inayopendekezwa na kuruhusu
mahakama ya kadhi,elimu inatakiwa kutolewa kwa makundi ya jamii
wakiwemo viongozi wa dini, serikali na wabunge kutokana na kutofautiana
kimtazamo juu ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo na katiba inayopendekezwa
ili kujenga taifa lenye umoja na kuvumiliana bila kujali tofauti ya
msingi ya dini,kabila na itikadi za kisiasa.
Kiongozi
wa kanisa katoliki parokia ya mavanga Padre Gafred Mwanyika amesisitiza
umuhimu wa kudumisha upendo na utayari wa kujitolea kuchangia na
kusaidia wahitaji na wasiojiweza huku kiongozi wa kanisa la agrikana
mtaa wa mavanga Padre Faraja Mapunda akihimiza wananchi kujiandikisha
kwa wingi katika Daftari la wapiga kura ili waweze kuwachangua viongozi
waadilifu na wanaojali maslahi ya taifa katika uchaguzi mkuu unaotarajia
kufanyika mwezi Oktoba Mwaka huu.
tiko
tiko
Post a Comment