tiko
tiko
Umoja
wa Makanisa mkoani Tanga umeishauri serikali kusogeza mbele zoezi la
kupiga kura ya maoni kuhusu rasimu ya pili ya katiba Pendekezwa kufuatia
muda wa mwezi mmoja uliotolewa kwa ajili ya wananchi kuisoma hautoshi
sanjari na nakala zilizotolewa kwa ajili ya wananchi kujisomea kuwa
chache.
Wakitoa tamko rasmi kwa serikali kuhusu zoezi la katiba
hiyo,viongozi wa madhehebu ya makanisa yote mkoa wa Tanga wamesema ni
vyema serikali ikasogeza mbele kabla ya siku ya mwisho ya mwezi April
haijawadia ili kutoa nafasi ya kutosha ya kuboresha Daftari la kudumu la
wapiga kura na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Aidha katika kikao hicho kilichoshirikisha viongozi wa makanisa
yote nchini mkoani Tanga baadhi yao walilalamikia mchakato wa kuanzishwa
kwa mahakama ya kadhi na kuiomba serikali ijenge umoja wa kitaifa kwa
kuimarisha Demokrasia zikiwemo za kidini kama alivyofanya mwasisi hayati
Mwalimu Jullius Nyerere.
Zoezi la kupiga kura ya maoni katika katiba pendekezwa nchini
linatarajiwa kufikia ukomo aprili 30 mwaka huu ambapo wananchi
walioingizwa katika Daftari kuu watapata fursa hiyo kwa kutumia
teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).
-Itv
tiko
tiko
Post a Comment