tiko
tiko
"Screen
shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog
uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania
tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo
mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini
mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.
Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza
kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote
lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha
ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine
kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na
BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure
kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo
wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari
zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.
Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli
hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari,
lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na
maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii
na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa
matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu
wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha
wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa
‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao
kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji
wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari
hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa,
TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), (https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na
mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza
kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha
za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi
wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja
kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua
hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha,
kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana
na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi
zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada
ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa
blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu
mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?”
wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana
wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi
Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha.... hili ndiyo tatizo kubwa la kila
mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed
journalist... UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka
kichefu chefu... full of attention-seeking sensationalism... utakuta
heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu
kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba
serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha
wandishi wa viblog uchwara.
Modewji blog tunaamini
pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo
kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI
MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu
likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
tiko
tiko
Post a Comment