tiko
tiko
Wakati
Rais Jakaya Kikwete akisema msimamo wa Jukwaa la Wakristo Tanzania
(TCF) wa kuwataka waumini wao kuipigia kura ya hapana Katiba
Inayopendekezwa ni wa hasira pia usiokuwa na tija kwa maendeleo ya
Taifa, baadhi ya maaskofu wameshikilia msimamo huo.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana
katika mkutano wa kamati ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam
iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini unaowajumuisha
viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo akilenga kuzungumzia tamko hilo
la TCF walilolitoa Machi 12, mwaka huu.
Katika tamko hilo lililosainiwa na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex
Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa
Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet liliwataka waumini wake
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapigakura na kuipigia kura ya hapana Katiba hiyo.
Jukwaa hilo lilitaja sababu mbili za
uamuzi wake huo kuwa ni Muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya
Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini na Kura ya Maoni kusababisha
mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini
wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu
vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa
wingi kupiga kura ya hapana,” lilisema tamko hilo.
Katika hotuba yake iliyodumu kwa saa
1.16, Rais Kikwete alianza kwa kuwaomba radhi viongozi hao kwa kuchelewa
kwa akisema alikuwa na majukumu mengi. Mkutano huo ulikuwa uanze saa
3.00 asubuhi lakini Rais Kikwete alifika saa 6.30 mchana.
Alisema “Taifa linapitia hali isiyokuwa
ya kawaida, tusipokuwa makini kuidhibiti itakuwa ni tatizo, ni kazi
kubwa inayohitaji moyo, uvumilivu na viongozi wenye kujali masilahi ya
Taifa.”
“Mwelekeo wa mambo hauhitaji uwe bingwa
kujua hali hairidhishi sana na kama hatutachukua hatua hatuwezi kufika
na tutasababisha uvunjifu wa amani za kidini na moto wake ni mkali
sana,” aliongeza Rais Kikwete aliyekuwa akizungumza kwa umakini na
taratibu.
Jukwaa la wakristo
Kuhusu tamko la Jukwaa la Wakristo, Rais
Kikwete alisema wakati Taifa likisubiri kuona mchakato wa Katiba
unakwenda hatua za mwisho kumekuwapo na matamko kadhaa ambayo
hayakumfurahisha.
“Nimeyasoma matamko hayo yote kwa
umakini, imenishangaza, imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa
nini wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga mkono,” alisema Rais
Kikwete aliyekuwa akizungumza kwa sauti ya chini wakati wote wa hotuba
yake.
“Kinachonisumbua ni kuipa sura na
mtazamo wa kidini Katiba Inayopendekezwa, kama ingekuwa inakinzana na
uhuru wa kuabudu hapo ingekuwa sawa lakini ibara ya 41 inatambua uhuru
wa kuabudu na kuitangaza dini, sasa katika mazingira hayo kuwaeleza
waumini kuikataa inanipa tabu sana,” aliongeza
tiko
tiko
Post a Comment