tiko
tiko
MTOTO aitwaye
Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya
kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa
kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Mwajuma
Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo jijini Dar, alisema aliishi na mwanaye
peke yake bila baba yake kwani walitengana Juni mwaka jana baada ya
kuishi bila kufunga ndoa kwa muda mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa
akimpeleka mwanaye nyumbani kwa wazazi wa mumewe kuwasalimia.
“Wiki iliyopita babu yake Eliyasa
alimuomba ili wakakae naye kwa muda mfupi, baada ya muda mfupi walimtuma
mtu akaniambia kuwa wameshamtahiri, nilishangaa sana kwa kuwa
hawakunitaarifu juu ya uamuzi huo, nikaenda kumuona lakini wakawa
wananikataza kumtazama sehemu za siri wakidai mila zao haziruhusu kwa
kipindi cha mwezi mzima.
Mtuhimiwa (mwenye fulana nyeupe) akiingia kituoni.
“Kutokana na shauku ya kutaka
kuthibitisha hilo, siku hiyo nilipofika tu nilimchukua na kumtazama hilo
eneo ndipo nikabaini kuwa alikuwa amekatwa katika kichwa, huenda huyo
ngariba hakuwa mzoefu, kamfanyia kienyeji lakini wengine wakisema huenda
walitaka kufanya mambo ya kishirikina,” alisema mama huyo.
Alisema baada ya kumkuta katika hali
hiyo, alianza kuhangaika naye hospitalini kutafuta msaada, alipofika
Temeke aliambiwa na madaktari.kwamba kijana wake alikatwa vibaya na
hivyo analazimika kufanyiwa upasuaji ili kumnusuru.
Babu wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi
la Polisi baada ya kufunguliwa shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala
Kizuiani kwa madai ya ukatili kwa faili namba UKATILI WA
MTOTO/MBL/RB/2251/2015 4/3/2015.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment