tiko
tiko
BAADA ya
tetesi kuzagaa kwamba Mtangazaji wa Clouds TV, Benny Kinyaiya anafanya
biashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo husafiri mara
kwa mara kinyemela kwenda Ulaya, mwenyewe amefungukia tuhuma hizo.
Akichati na gazeti hili juzi akiwa
nchini Uingereza, Benny alisema kuwa anashangazwa na madai hayo kwani
hajawahi na wala hafikirii kufanya biashara hiyo.
“Hizo taarifa ni za uongo kabisa, ni
kweli nasafiri mara kwa mara na hata sasa niko Ulaya kwa biashara zangu
binafsi lakini hilo la unga siyo kweli, ni uzushi tu. Kuna mambo yangu
ya kibiashara nakuja kufanya ambayo siwezi kuyaanika,” alisema Benny.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment