tiko
tiko
Stori: Mwandishi Wetu
Sifa za kitaaluma (CV) za mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Vick Kamata zilizopo kwenye tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania, zimezua utata kutokana na ‘makengeza’ zilizonazo.

Habari
zilizotua kwenye dawati za Uwazi Mizengwe kutoka kwa chanzo chetu kabla
ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zilieleza kuwa sifa za
kitaaluma za mbunge huyo zilizoandikwa kwenye mtandao wa bunge, zilikuwa
na dalili ya kupotosha baadhi ya mambo.
Uwazi
Mizengwe liliingia mzigoni na kubaini kuwa CV hiyo ya Mheshimiwa Vick,
ilikuwa ikionesha kwamba mheshimiwa huyo ana shahada ya pili (masters
degree) katika mambo ya utawala na biashara za kimataifa aliyoipata
kwenye Chuo Kikuu cha Southampton Solent cha nchini Uingereza kuanzia
mwaka 2008 hadi 2009.
Pia
CV hiyo ilionesha kwamba shahada ya kwanza ya uandishi wa habari
(bachelor degree) aliipata kwenye Chuo Kikuu cha St. Augustine jijini
Mwanza kuanzia mwaka 2001 hadi 2005. Kabla ya hapo, alikuwa na
stashahada (diploma) ya mambo ya kompyuta.
MKANGANYIKO ULIOPO
Katika CV hiyohiyo, kuna maelezo mengine yanayokinzana na ya awali ambayo yanaeleza kwamba mheshimiwa huyo, hana shahada ya uandishi wa habari bali alisomea kozi fupi ya uandishi wa habari (certificate) katika chuo hicho kilichopo jijini Mwanza kuanzia mwaka 2000 hadi 2001.

Mkanganyiko
mwingine uliopo, ni kwamba kama ni kweli mheshimiwa huyo hakuwa na
shahada ya kwanza ya uandishi wa habari, isingewezekana kwenda kuchukua
shahada ya pili nchini Uingereza kwani kisheria, ni lazima uwe na
shahada ya kwanza ndiyo ukasomee ya pili.
“Haiwezekani
mtu mwenye diploma (shahada) tena ya kawaida tu aende kuchukua masters,
ni lazima awe kwanza na digrii au advanced diploma,” alichangia mdau
mmoja wakati akichangia mada hiyo mtandaoni.
Baada
ya kujiridhisha juu ya mkanganyiko huo, Uwazi Mizengwe lilimtafuta
mbunge huyo ili atoe ufafanuzi lakini simu yake ya mkononi haikuwa
ikipatikana hewani. Juhudi za kumtafuta bado zinaendelea na
atakapopatikana, atatoa ufafanuzi kuhusu mkanganyiko huo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment