tiko
tiko
Nitakuwa sijakosea nikimuita Shilole
kama mjasiriamali, kwa sababu ni mwanamke mtafutaji, siyo kama wale
akina dada wanaouza sura mijini, kipato chao kikubwa wakitarajia kutoka
kwa wanaume.
Huyu mdada ni shoka, anajichanganya kila
sehemu ili mradi ‘chapaa’ iingie kibindoni, ndiyo maana leo utamuona
kwenye filamu, kesho unakutana naye jukwaani anazungusha kiuno kama hana
akili sawasawa, hiyo yote ni katika kuwapa mashabiki kile wao
wanapenda, ili mwisho wa siku mkono wake uende kinywani.
Shilole anavuma zaidi kimuziki kwa
sababu amefanya kazi nyingi na nzuri, kiasi kwamba amewahi kupata
mialiko sehemu mbalimbali, ndani na nje ya nchi. Kibao chake kilichompa
heshima kubwa kinaitwa Malele, ingawa pia aliwahi kuimba Bata Batani
aliomshirikisha Abdul Kiba na Nakomaa na Jiji kuzitaja chache.
Binti huyu mwenyeji wa Mkoa wa Tabora
anafanya vizuri kwa sababu aina ya muziki alioamua kuufanya, uko na watu
wachache kwa hiyo upinzani si mkubwa. Wapinzani wake ni kama akina IT,
Snura na wengine wachache.
Nje ya muziki, Shilole ni binadamu kama
binadamu wengine, akifanya yale ambayo mimi na wewe tunafanya. Hata
hivyo, uhusiano wake wa kimapenzi na Nuh Mziwanda umekuwa ukikosolewa na
wapinzani wake, kwa madai kwamba yeye ni mkubwa kiumri kuliko mwenzake.
Binafsi nimewahi kumuuliza swali hilo,
kama ni kweli wanavyosema kuwa ‘anambembenda’ bwana mdogo, lakini jibu
lake kama inavyokuwa mara zote, ni kwamba Nuh ni mtu mzima na kwa maana
hiyo, waachwe waendelee na maisha yao.
Ni kweli, Nuh anaweza kuwa ana umri
mdogo kuliko Shilole, lakini ni mtu mzima anayejitambua, kwa hiyo kama
ameamua kuwa na mwenza anayemzidi umri, ni uamuzi wake ambao ni makosa
kumkosoa, mbona wababu wengi tu wanawaoa ‘wajukuu’ zao?
Lakini katikati ya kelele hizi, yapo
madai ya mara kwa mara juu ya kuwepo kwa mizozo inayosababisha wawili
hao kupigana, ingawa habari zinasema inapotokea hivyo, binti huyo ndiye
anaibuka kidedea kwa kushinda pambano.
Kwetu sisi waandishi, ugomvi kati yao
siyo kitu kigeni. Kinachosikitisha, mara zote Shilole ndiye anatajwa
kuwa chanzo na mshindi wa kila tukio. Ninajua maisha ya ndoa yalivyo na
hivyo ninaelewa ni kwa kiwango gani haipendezi habari za uhusiano wao
zinapotapakaa nje. Ninafahamu juu ya uwepo wa kutokuelewana ndani ya
uhusiano wa watu wengi, lakini ni wengi pia hatusikii habari zao
zikitoka nje.
Kwa Shilole na Nuh, watu wanamsema
vibaya mwanamke, wakisema anamuonea mwenzake kwa vile tu, yeye mambo
yake ni mazuri kuliko mwenzake. Nuh ambaye pia ni msanii, hana fedha
kama Shishi Baby.
Kiukweli, hatuwezi kujua nini hasa
kinatokea ndani mwao, lakini maneno ya aina ileile yanapoendelea
kutolewa juu ya watu walewale, yanatosha kutuma ujumbe kuwa lisemwalo
lipo na kama halipo laja.
Kama mwanamke, kama staa, hatoi picha nzuri kwa jamii inayomzunguka, ambayo inaamini katika mila na desturi za Kitanzania. Asiilazimishe jamii yake kuelewa kwamba anakuwa mgomvi kwa sababu tu anaringia uwezo wake kifedha.
Kama mwanamke, kama staa, hatoi picha nzuri kwa jamii inayomzunguka, ambayo inaamini katika mila na desturi za Kitanzania. Asiilazimishe jamii yake kuelewa kwamba anakuwa mgomvi kwa sababu tu anaringia uwezo wake kifedha.
Sina uhakika wa wingi wa fedha
alizonazo, lakini ninachoamini ni kwamba mwanamke wa kiafrika siku zote
anapaswa kuwa na heshima kwa mume au bwana aliyeamua kuwa naye. Hela
haina mwenyewe, leo unayo kesho hauna, kama unaamini katika uwezo
kifedha, maana yake ni utumwa.
Kesho na keshokutwa hela ikiondoka,
utakuwa tayari kunyanyasika kwa vile unaamini katika mkwanja, kitu
ambacho siyo kweli. Utu na heshima kwanza!
tiko
tiko
Post a Comment