tiko
tiko
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dr. Willbroad Slaa, ameripoti katika Kituo cha
Polisi Central kilichopo Posta jijini Dar kuhusiana na sakata zima la
mlinzi wake anayetuhumiwa kutaka kumuua.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo, Slaa alisema yeye hakuitwa na
Jeshi la Polisi kujielezea bali kutokana na maneno yanavyozidi kusambaa
na kuwasilishwa ndivyo sivyo ameona aende kueleza ukweli ulivyo.
Alisema kuwa, kwa mujibu wa chama chake, ameona ni vyema kwenda
kulieleza Jeshi la Polisi kuhusiana na ishu nzima inayomkabili mlinzi
wake, ambapo alikutana na Kamanda wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam,
Suleimani Kova na kumueleza kila kitu kwa kuandika karatasi tisa (9)
zenye maelezo yake, hivyo zoezi zima la kutoa taarifa kuhusiana na
alichoandika ameliachia Jeshi la Polisi baada ya wao kufanya kazi yao ya
Uchunguzi.
“Ndugu zangu wanahabari sijaitwa hapa kwa ajili ya mahojiano kama
taarifa zinavyozaga lakini kutokana na uongozi nilionao nimeona ni vyema
suala hili nilifikishe Polisi, na katika maelezo yangu nimeweza
kuandika zaidi ya karatasi tisa (9) zenye ukweli mtupu, hivyo
nimelikabidhi Jeshi la Polisi na baada ya wao kufanya uchunguzi litatoa
taarifa kamili juu ya kile nilicho kiandika,’’ alisema Dr. Slaa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment