tiko
tiko
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James
Mbatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusu kuendelea kwa ajali za barabarani. Picha na Venance Nestory
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi taifa ,James Mbatia amesema kwamba ajali iliyotokea
eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa ilikuwa imepangwa na binadamu
na wala sio mipango ya Mungu.
Akizungumza jijini leo Mbatia amesema
ajali hiyo ilipangwa na watendaji wa serikali kwa sababu ajali hiyo
ilisababishwa na shimo kubwa ambalo limekaa kwa muda mrefu eneo hilo
pasipo juhudi zozote za Serikali kulikarabati.
Mbatia amesema hawezi kukaa kimya ni
lazima awasilishe suala hili bungeni ili wahusika wachukuliwe hatua kwa
kuacha shimo kubwa barabarani kwa muda mrefu bila kuliziba.
Amesema shimo hilo ambalo ndio hasa
lilikuwa chanzo cha ajali hiyo ni la muda mrefu lakini viongozi wa
serikali wanaliangalia tu bila kuchukua hatua ya kuliziba.
‘’Jamani watanzania waliopoteza maisha
kwenye ajali hiyo ni wengi na ni aibu kwa taifa, ukizingatia chanzo
cha ajali hiyo ni shimo la muda mrefu ambalo linaangaliwa na viongozi
wetu kila siku bila kuliziba’’alisema Mbatia
Amesema ajali hudokeza kwa ujumla
matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio
yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya
tukio.
Amesema madereva wanaoendesha magari ya
abiria wanatakiwa kupelekwa shule angalau kwa miezi sita ikiwa ni pamoja
na kupimwa afya mara kwa mara.
Aidha ameitaka serikali kutoa tamko
kuhusu ajali hiyo na sio kukaa kimya mpaka waanze kupigiwa makelele na
wananchi kupitia vyombo vya habari.
Watu zaidi ya 40 waliokuwa kwenye basi
la kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar
es Salaam, walifariki papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea jana
wengine 23 wakijeruhiwa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment