tiko
tiko

Serikali
imesema asilimia tano kati ya 17 inayochangiwa na wahisani wa maendeleo
katika bajeti ya mwaka huu imeathirika kutokana na sakata la uchotwaji
wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Waziri
wa Fedha, Saada Mkuya Salum (pichani), alitoa kauli hiyo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya
mkutano kati ya serikali, wadau na wahisani wa maendeleo kwa nchi
zinazoendelea.
Lengo
la mkutano huo ni kufanya majadiliano ili kufahamu mwenendo mzima wa
bajeti ya serikali ulipofikia na maeneo yanayohitaji kurekebishwa.
Mkuya
alisema kutokana na sakata la Escrow lililojitokeza baada ya bajeti
kupitishwa, wameona ipo haja ya kuangalia upya mfumo mzima na mikakati
yao ya utekelezaji wa bajeti hiyo ili kujua kama bado itaendelea kuwa
hai katika utekelezaji wake.
“Katika
hili tumeona upo umuhimu wa kutazama upya makubalianao na misingi yetu
kama imepoteza uhalisia kiutendaji au la ili kujua tutaendeleaje nayo
hata baada ya kujitokeza kwa jambo hili,” alisema.
Aliongeza
kuwa kutokana na hatua stahiki na za wazi zilizochukuliwa na serikali,
wahisani wameridhika na wataendelea na utekelezaji wa kuchangia bajeti
hiyo kama walivyokubaliana.
“Si
vyema bajeti ya serikali iathirike kutokana na mambo yanayojitokeza, na
hivi sasa fedha tutakazopata tutazielekeza katika maeneo ya barabara,
maji na nishati kama ilivyopendekezwa,” alisema.
Alisema
wiki mbili kuanzia sasa takribani Dola milioni 44 (zaidi ya Sh. bilioni
50) huku Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika wakijipanga
kutoa Dola millioni 227 (Sh. bilioni 409).
Alisema
nchi zinazoendelea zinakabiliwa na masharti magumu katika kupewa
misaada, hivyo uwapo utaratibu maalum wa upokeaji wa misaada ili
kuepusha kukwama pindi matatizo yanapojitokeza baada ya makubalinao na
wahisani.
Naye
Balozi wa Finland nchini, Sinikka Antila, alisema wataendelea kutoa
misaada kama walivyoahidi baada ya kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa
na serikali dhidi ya wote waliohusika katika sakata la Tegeta Escrow.
“Kutokana
na hotuba ya Raisi Kikwete ya Disemba 22, mwaka jana, tumeona jitihada
za wazi zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya wahusika wa sakata la
Escrow, hivyo tutaendelea kuchangia bajeti kama kawaida,” alisema
Antila.
Wahisani
wa maendeleo wanaochangia bajeti ni Canada, Denmark, Finland,
Ujerumani, Ireland, Japan, Sweden, Uingereza, Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment