tiko
tiko
Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na
tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook
accounts kwa majina mbalimbali kama Justin Stan, James
Brown,Onesmo,Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na
mengineyo mengi.
Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook
Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya
friends request kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa
akiwaambia marafiki zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu
mbali mbali tofauti katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano
kwingine akidai anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya
Tanesco Makao Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi
kwamba ana watu wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa
sharti la wanaotaka kazi kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na
wakilipa kiasi cha shilingi 50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za
kazi hizo.
Wakati mwingine amekuwa akiwa wadanganya
baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au akihudhuria semina na kwamba
mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama shilingi 25,000 au 30,000 na
kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi atawarudishia mara atakapokua
free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za simu mojawapo zikiwa hizi
0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka amekuwa akiwatukana matusi
makubwa ya nguoni bila uoga.
Natoa tahadhari kwa watu wote
kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua, kuzingatia umakini
haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii ni wengi sana
online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa design hii
basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa kumnasa.
Vijana tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu
na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna hadithi yeyote niliyowahi
kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia ya mkato. Mwana fundi
ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie ajira.
Mwisho naomba marafiki zangu wooote
mnisaidie kurepost message hii kwani naamini itawaokoa wengi
(vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa hawajui
utapeli huu wa online.
Picha hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za facebook.
Mimi ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana
Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia kwa namna ya kipekee nawashukuru
wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda wao kunitafuta na kunipa taarifa
hizi muhimu walipomshtukia Tapeli huyu.
Mwenyezi Mungu awabariki saana.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment