tiko
tiko
BAADA ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel
kujifungua, mwanahabari wetu ametia timu nyumbani kwa Aunt na
kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na
taarifa za kujifungua si za kweli.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua
kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video
kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande cha
video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote ambapo
mashabiki wake walimiminika na kuanza kumpongeza wakijua tayari
kajifungua.
Hapa chini ni kipande cha video alichoweka Aunt Ezekiel kwenye akaunti yake ya Instagram.
Find more videos like this on Global Publishers
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment