tiko
tiko
JAMAA aliyetambulika
kwa jina moja la Jacob, mkazi wa Majengo wilayani Misungwi, Mkoani
Mwanza, amejikuta yuko mikononi mwa polisi wakati akifanya jaribio la
wizi wa fedha sh. 70, 000 kupitia huduma za fedha za mtandao wa simu.
Jamaa
huyo amefanya tukio hilo hivi karibuni maeneo ya Misungwi Stand ambapo
aliingia dukani kwa wakala Robert Bukoli na kuomba awekewe fedha hizo,
wakala alichukua namba yake ya simu ili amuwekee fedha hizo.
Chanzo
makini kilichokuwepo dukani hapo kilidai kuwa, wakati Bukoli akiendelea
kuingiza namba za simu za mteja huyo kwenye simu yake, alimuomba mteja
huyo aweke fedha hizo taslim mezani ili itakapoingia kwake (mteja) naye
wakala awe na chake mkononi ndipo mteja huyo alianza kuhaha.
Wakala
aliendelea kumsisitiza mteja huyo aweke pesa mezani lakini mteja huyo
alianza kuonesha dalili za kukimbia ndipo aliamua kumshikilia na kupiga
simu polisi ambapo alikamatwa na kupelekwa kituoni.
“Inaonekana mpango wake alikuwa anataka awekewe fedha kisha azuge kama anaongea na simu, atimke bahati nzuri wakala naye alishamshtukia,” kilisema chanzo hicho.
“Inaonekana mpango wake alikuwa anataka awekewe fedha kisha azuge kama anaongea na simu, atimke bahati nzuri wakala naye alishamshtukia,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumzia
sakata hilo, wakala huyo alisema alianza kumtilia shaka jamaa huyo
baada tu ya kufika dukani kwake.“Jamaa nilimtilia shaka mapema alipofika
dukani maana alianza kuongea na mtu mwingine kwenye simu kwa muda mrefu
kabla hajaniambia nimuwekee pesa baadae ndio akasogea na kuniambia ana
haraka nimuwekee pesa upesi.
“Nikachukua
namba yake ya simu, nikiwa naijaza kwenye simu yangu nikamwambia naye
aweke pesa mezani lakini hakufanya hivyo, nilipo msisitiza zaidi jamaa
nikamwona anaingiwa na hofu na akataka kukimbia ndipo nikamshika na
kupiga simu polisi akakamatwa, nilipofuatilia kituoni nikakuta ana kesi
nyingine ya kuuza kiwanja mara mbili hivyo inasemekana alitaka
kunitapeli hizo pesa ili akalipe deni lake la kesi ya nyuma,” alisema
wakala huyo ambapo alimuacha mtuhumiwa kituoni kwa ajili ya taratibu za
kisheria.
tiko
tiko
Post a Comment