tiko
tiko
KUFUATIA madai
kuwa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu, jamaa na
marafiki kibao walijazana nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es
Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi, lakini walipokuta habari tofauti
walimvaa na kumlaumu kwa kuwadanganya.
Jumatano
usiku katika mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Aunt Ezekiel
ambaye ni mke wa mtu aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela, alitupia
picha ikimuonyesha akiwa na kitoto kichanga, ambacho watu wengi
waliamini ni wa kwake, hasa kwa vile katika siku za hivi karibuni
ameonekana kupunguza mitoko.
Watu
wa karibu wa muigizaji huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi
na mcheza shoo wa Diamond Platnumz aitwaye Iyobo, walikwenda nyumbani
kwake kwa ajili ya kumpongeza, lakini walipatwa na mshangao baada ya
kumkuta akiwa na tumbo lake kama kawaida.
“Sisi
tulijua mwenzetu amejaaliwa kujifungua salama, sasa jambo la kushangaza
wenzake tumekuja kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa, hivi
aliwaza nini kuweka picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa
kinachoendelea,” shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili
nje ya nyumba yake, lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.
Mmoja
wa marafiki waliodaiwa kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt,
alikuwa ni shosti yake Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa
mapema kuhusu ukweli wa ishu hiyo.
“Nilishtuka
kweli, nikasema inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye
mitandao ya kijamii? Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya
fair bwana,” alisema Aunt.Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia
mwezi wa saba, hivyo wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata
kiumbe njiti.
tiko
tiko
Post a Comment