tiko
tiko
HUKU maelfu
ya Watanzania wakiamini kwamba, kifo cha aliyekuwa mbunge wa Mbinga
Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba ndiyo kile kilichotabiriwa
na mnajimu Maalim Hassan Hussein Yahya, mwenyewe ameibuka na kusema
sicho!
Akizungumza
na Risasi Jumamosi katikati ya wiki hii jijini Dar, Maalim Hassan
alisema kuwa, baada ya kifo cha Kapteni Komba ambaye alikuwa pia
mwanasiasa mkubwa nchini, wengi wameamini utabiri wake alioutoa mwanzoni
mwa mwaka huu kwamba kuna mtu maarufu mwanasiasa atafariki dunia
ghafla, basi ndiye Komba.
“Kwanza
nataka watu wajue siyo Komba. Yule mwanasiasa niliyemtabiria mimi yuko
palepale. Yeye ataanguka jukwaani na atafariki papo hapo,” alisema
Maalim.
Aliongeza
kuwa, kifo cha Komba ni upepo wa mauti tu lakini hayumo katika matukio
ya utabiri wake wa mwaka 2015 ambapo alichambua vizuri hali ya kisiasa
nchini. Katika utabiri wake huo, Maalim Hassan alisema mwanasiasa huyo
atakuwa mgombea wa urais (hakumtaja jina lake wala la chama) ambapo
atapatwa na mauti hayo akiwa anahutubia jukwaani kwa ajili ya kampeni.
Kwa
madai hayo, wengi walisema ni Komba kwa sababu katika kipindi cha kifo
chake alikuwa anajiandaa na kampeni za ubunge jimboni mwake na pia
alikuwa anajiandaa na nyimbo za kampeni za kuhamasisha upigaji kura
mwaka huu.
tiko
tiko
Post a Comment