tiko
tiko
Mbunge
wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige, amesema kuna watu walifukiwa wakiwa
hai wakati wa uanzishaji wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu mkoani
Shinyanga.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo bungeni
leo alipokuwa akiuliza swali la nyongeza. Maige alihoji serikali
inasemaje kuhusu kuwalipa fidia ndugu wa watu hao.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Charles Kitwanga alisema yeye alikuwa ni mmoja wa
watu waliokuwa wakichimba madini katika eneo hilo kati ya mwaka 1984 na
1985.
Alitaka mbunge huyo kupeleka ushahidi kwake ambao ni tofauti na ushahidi ambao wamewahi kupokea awali.
Katika swali la msingi, Maige alihoji ni
hatua gani wamefikia katika kufanyia kazi maombi ya wananchi
waliokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa mgodi huo ya kulipwa fidia na mali.
Akijibu swali hilo, Kitwanga, alisema
wakati wa kuanzishwa kwa mgodi huo hakuna kaya yoyote iliyostahili
kulipwa fidia kwasababu hakuna mtu aliyefukuzwa katika kijiji cha Kakola
ambako ndiko makazi rasmi ya watu.
“Iwapo mgodi unahitaji kutumia eneo la
kijiji hicho ungelazimika kufidia wananchi wote ambao wangetakiwa
kupisha ujenzi wa mgodi kulingana na sheria za nchi,”alisema.
tiko
tiko
Post a Comment