tiko
tiko
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa jeshi la magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa ni pamoja na sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).
Akitoa
taarifa za kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa polisi mkoani hapa
Naibu Kamishina, Charles Mkumbo alisema kuwa askari hao walikamatwa juzi
majira ya saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi
Wilayani Bariadi.
Mkumbo
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba H 2420 PC Seleman
Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani
Simiyu, na askari namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari
Magereza wilayani Bariadi.
Kamanda
Mkumbo alieleza kuwa baada ya askari hao kukamatwa mmoja wao PC
Selemani Juma alipopekuliwa katika mfuko wa suruali yake alikutwa na
noti zingine za Bandia za elfu kumi kumi na jumla yake kama zingelikuwa
halali zingelikuwa na thamani ya Shilingi 1,920,000.
Alisema
kuwa askari hao walifika kwenye kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na
pikipiki yenye namba za usajili T 403 CXW aina ya Sunlg kwa lengo la
kuweka fedha hizo kwenye simu.
Baadhi ya noti bandia walizokutwa nazo
Naibu
kamishna wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo akiwaonyesha
waandishi wa habari baadhi ya pesa bandia ambazo zilikamatwa na askari
wa jeshi la polisi
Sare zilizokamatwa.
tiko
tiko
Post a Comment