tiko
tiko
Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limekamata gari la kampuni ya Wengert Windrose
safari inayojihusisha na uwindaji wa kitalii katika maeneo mbalimbali
nchini likiwa linasafirisha madawa ya kulevya aina Bangi.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema madawa hayo kiasi
cha magunia 11 yamekamatwa katika wilaya ya Longido majira ya saa tano
usiku yakisafirishwa kwenda nchi jirani kwenye gari namba T695 ARR
mali ya kampuni ya Wengert Safaris ikiwa inaendeshwa na dereva wa
kampuni hiyo aliyetajwa kwa jina la Frank Faustine.
Kamanda
Sababs amesema polisi walilitilia shaka gari hilo ambalo kwa kawaida
linajulikana kuwa linabeba wageni na baada ya kufanya upekuzi ndipo
wakagundua kuwa kilichobebwa kwenye gari hilo sio wageni bali ni madawa
hayo ya kulevya aina ya Bangi.
Akizungumzia
tukio hilo meneja maendeleo ya jamii wa kampuni hiyo ya Wengert
safaris Bi Aurelia Mtuy amesema madawa yaliyoakamtwa ni mali ya dereva
na wala sio mali ya kampuni na amelishukuru jeshi la polisi kwa hatua
hiyo ambayo pia imeisaidia kampuni kubaini maovu yanayofanywa na baadhi
ya madereva wao.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi pamoja na kulipongeza jeshi la polisi
kwa hatua hiyo wameitaka serikali na idara zinazohusika kupanua wigo wa
kuweza kubaini mbinu mpya za kihalifu hasa wa usafirishaji wa madawa
kwani wana mtandao mkubwa ukiwemo ya kutumia magari ya makampuni, watu
maarufu, na taasisi zikiwemo za serikali.
tiko
tiko
Post a Comment