tiko
tiko
Aliyewahi
kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Warioba,
ametaja sifa za rais ajaye kuwa ni uzalendo, uadilifu na dira katika
kuliongoza taifa.
Jaji Warioba alisema hayo juzi, katika Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani na ITV.
“Rais anapaswa pia kujua matatizo ya
Watanzania, awe mzalendo, mwadilifu na aone mbali. Anapaswa pia kujua
atafanya nini kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta za afya na
uchumi,” alisema.
Kwa kauli hiyo, Jaji Warioba anaungana
na viongozi wengine kadhaa waliowahi kuzungumzia sifa za rais ajaye,
akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Hassy
Kitine; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye; Mwanasiasa
mkongwe, Cleopa Msuya; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba; na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk
Emmanuel Nchimbi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
viongozi hao walitaja sifa hizo za rais ajaye kuwa ni uadilifu, busara,
uzalendo, uwezo wa kufanya uamuzi na kuyasimamia, weledi wa masuala ya
maendeleo, kutokuwa na makundi, kuwa na nguvu ya mwili na akili na uwezo
wa kusimamia Katiba na sheria za nchi.
Walisema yeyote asiyekuwa na sifa hizo, hafai kuwa rais na kuwaongoza Watanzania.
Dk Kitine: Urais siyo lelemama
“Mtu anayetangaza (mwenyewe) kuwa
anataka kuwa rais anakuwa hajui anachokisema..., anakuwa hajui matatizo
ya urais. Mtu asiyejua matatizo ya urais anaweza kujisemea tu kwa sababu
haelewi urais maana yake ni nini,” alisema aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Idara ya Usalama wa Taifa na Waziri wa kwanza wa Ofisi ya Rais (Utawala
Bora), Dk Hassy Kitine.
Kitine alisema hayo Septemba 9 mwaka
jana. Alisisitiza, “Mtu anayejua maana na changamoto za urais hawezi
kutangaza anautaka urais. Ataogopa kwa sababu ya changamoto (nyingi) za
urais…, kwa hiyo hawezi kujitangazia ovyo kuutaka.”
Kwa mujibu wa Dk Kitine anayetaka kuwa
rais lazima awe mwadilifu wa asili na siyo wa kujifanya. Awe pia
mzalendo na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi.
“Rais awe amesoma na asiwe na kundi, pia
ajue misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na aonekane kuwa
anachukia rushwa kwa vitendo.
tiko
tiko
Post a Comment