tiko
tiko
HATIMAYE siri
ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuhamia kwenye mjengo
wake wa kisasa uliyopo Tegeta -Madale jijini Dar imevuja huku ikitajwa
kuwepo na vionjo vya ushirikina.
Chanzo makini kimeliambia Amani kuwa,
licha ya kumalizika kwa mjengo huo, lakini Diamond alikuwa akikataa
kuhamia kutokana na umbali kutoka huko hadi mitaa aliyoizoea lakini
shinikizo lilikuja kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Zarina Hassan ‘Zari’
ambaye tangu aliponasa ujauzito amekuwa akitamani kuwa karibu na mpenzi
wake huyo ila ilikuwa ikishindikana kufuatia mazingira aliyokuwa
akiishi mwanzo Diamond, Sinza-Mori, Dar.
“Ndugu yangu kama unataka kufahamu
undani zaidi wa hiki ninachokueleza muulize Diamond mwenyewe atakwambia,
Zari siku zote alikuwa akitaka kuwa karibu na Diamond, hasa baada ya
ujauzito lakini ndugu zake walikuwa wakimkatalia kufanya hivyo kwa
kuhofia mimba yake kuchoropoka kutokana na vijicho vya watu.
Mpenzi wa Diamond Platinumz, Zarina Hassan ‘Zari’ akiwa katika mjengo huo.
“Kingine kilichokuwa kikimfanya Diamond
ashindwe kumruhusu Zari kuwepo makazi ya awali ya Diamond ni mama yake
alipougua, si unajua ilidaiwa yalikuwa ni mambo ya kishirikina?“Amini
usiamini kutokana na mambo hayo, ilibidi Zari amwambie Diamond
akamilishe nyumba yake haraka iwezekanavyo ili tu aweze kuhamia na yeye
aje kukaa maana tangu awe mjamzito mara kadhaa amekuwa akitamani sana
kuishi na Diamond,” kilisema chanzo hicho.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Diamond
laivu ili aweze kuyaweka sawa madai hayo ambapo baada ya kupatikana
alijibu hivi:“Kaka, hayo maneno wewe achana nayo maana kila mtu anaongea
anachokifahamu, isitoshe yanaongewa mengi kwa kuwa wanajua nimehama
Sinza. Ila ninachoweza kusema kila jambo linapangwa na Mungu hivyo sina
uwezo wa kuwazuia watu kusema wanachojisikia.”
Jumamosi
iliyopita, Diamond alikata shauri na kuhamia kwenye makazi yake
mwenyewe baada ya ujenzi wa miaka karibia mitatu. Kwa mujibu wa
mkandarasi mmoja, nyumba hiyo mpaka kukamilika kwake, imetafuna karibu
shilingi milioni mia nne (400,000,000).
tiko
tiko
Post a Comment