tiko
tiko
Akiuliza swali bungeni leo, Rwamlaza alihoji serikali inasemaje kuhusiana madai hayo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima, alisema Sheria za Usalama wa
Barabarani namba 67 ya mwaka 1973 inatoa mamlaka kwa askari wa
barabarani kutoza faini za papo kwa papo kwa makosa mbalimbali ya
usalama wa barabarani.
“Hili ni moja ya jukumu la msingi la
kikosi cha usalama wa barabarani unaolenga kuimarisha usimamizi wa
Sheria za Usalama wa Barabarani,”alisema.
Alisema ukamataji wa makosa ya
barabarani na faini ya papo kwa papo hulenga katika kuwatia hofu ya
adhabu madereva wakorofi hivyo kuwafanya wafuate sheria na kanuni za
usalama barabarani.
“Hakuna kiwango cha pesa ambacho askari
wa usalama wa barabarani amepangiwa kukusanya, askari ameelekezwa
kukamata makosa kwa wingi iwezekanavyo hususani makosa hatarishi kama
vile mwendo wa kasi, ulevi, ujazaji wa abiria na mizigo, uendeshaji wa
hatari na kadhalika,”alisema.
Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti
Maalum , (CUF), Mkiwa Kimwaga, alisema askari wa vitochi barabarani
wamekuwa ni kero kubwa kwa madereva.
“Wakati mwingine wanasimamisha magari kama sita na wanakwambia kuwa na wewe umekuwa ukiendesha katika mwendo kasi,”alisema.
Alihoji ni lini serikali itanunua
vitochi vya kisasa ambavyo vitatoa na namba badala ya vya sasa ambavyo
vinaonyesha mwendo tu kama walivyoahidi katika bajeti iliyopita.
Akijibu swali hilo, Silima alisema wananchi hawatakiwi kuona kero kwa vitochi kwa sababu viko pale kwa ajili ya kuepusha ajali.
“Fikra kwamba vitochi ni kero mziondoe kabisa, tunakerwa ili tusife tunataka maisha yenu yaendelee,”alisema.
Alisema ajali nyingi zinazotokea nchini
zinasababishwa na mwendo kasi. Hata hivyo, alisema serikali imeshanunua
baadhi ya kamera za kisasa zinazoonyesha namba za gari.
tiko
tiko
Post a Comment