tiko
tiko
Leo tunaendelea na uchambuzi wa Mkoa wa Tanga kwa kuangalia majimbo ya Handeni, Korogwe Mjini na Korogwe Vijijini.
Jimbo la Handeni linagusa eneo lote la
Wilaya ya Handeni. Jimbo hili lina mji mmoja na maeneo ya vijijini. Eneo
la Mjini ni pale Handeni Mjini ambako kuna kata 12 na mitaa 60 na
maeneo ya vijijini yanayounda wilaya hii ni kata 20, vijiji 91 na
vitongoji 775.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Handeni kuna wakazi 276,646.
Majimbo ya Korogwe Mjini na Korogwe
Vijijini yako Wilaya ya Korogwe na ndiyo yanayotengeneza Wilaya hii
yenye kata 20, vijiji 118 na vitongoji 610, huku ikiwa na wakazi
242,038.
Jimbo la Handeni
Kuna watu hukaa vijiweni na kusema kuwa
CCM inakufa kirahisi. Jambo hili ni la mjadala mpana, ukitaka kuona bado
CCM iko hai, nenda Handeni upime maneno yangu.
Jimbo la Handeni limeweka rekodi muhimu
kwa CCM tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Ni jimbo
linalostaajabisha kwa namna wananchi wake walivyo wavumilivu na watiifu
kwa chama hicho.
Mwaka 1995 wakati mfumo wa vyama vingi
unaanza, CCM haikufanya ajizi, ilijipanga kwa kutumia mtandao wake imara
na ikampata mgombea imara, Dk Abdallah Omar Kigoda. Dk Kigoda ambaye
kitaaluma ni mtaalamu wa uchumi na kilimo akiwa amepata shahada yake ya
kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975, Shahada ya Uzamili
kutoka Chuo Kikuu cha Vanderbilt (Marekani) mwaka 1980 na shahada ya
uzamivu katika masuala ya Uchumi wa Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha
Missouri Colombia, ndiye aliyepewa baraka zote na CCM kupambana na
wapinzani.
Mipango ya NCCR na vyama vingine
vilivyokuwa na mwamko wa mageuzi wakati huo haikuwa na tija kubwa kutoa
ushindani baina ya vyama hivyo na CCM. Mwishowe Kigoda aliwashinda
wapinzani wake na akakabidhiwa kiti cha ubunge wa Handeni kwa mara ya
kwanza tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi.
Rais Benjamini Mkapa alimteua kuwa
Waziri wa Viwanda na Biashara tangu mwaka 1995 – 1996, kisha
akahamishiwa Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1997 – 2000.
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2000, Kigoda
akiwa Waziri na Mbunge aliyemaliza kipindi cha kwanza, akapewa tena kazi
na wana CCM kuifanya Handeni iendelee kuwa chini ya chama hicho.
Akajitosa na kukutana na upinzani dhaifu, akashinda kwa kura nyingi na
kuchaguliwa kuwa mbunge kwa kipindi cha pili.
Rais Mkapa pia akamwongeza mzigo wa
uwaziri, mara hii akipangiwa Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji
(kuyashughulikia mashirika ya umma ambayo kwa mujibu wa Mkapa, yalikuwa
mzigo kwa Serikali yake). Dk Kigoda alidumu kwenye wadhifa huu hadi
mwaka 2005 ulipokoma uongozi wa Mkapa
tiko
tiko
Post a Comment