tiko
tiko
Matukio ya utekaji watu yamekuwa yakitokea duniani kwa miaka nenda rudi, huku wahusika wa utekaji wakitoa masharti wanayotaka yatekelezwe ili kuwaachia mateka.
Miongoni mwa madai wanayotaka yatekelezwe ni kulipwa kiasi cha fedha ambacho kwa kawaida huwa kikubwa.
Utekaji watu ni hali inayozua hofu na
sintofahamu miongoni mwa jamii kutokana na ukweli kwamba mara nyingi
huambatana na mateso, unyanyasaji kwa waliotekwa hata wakati mwingine
kuuawa.
Vitendo hivyo vya kinyama, mara nyingi huhusishwa na chuki au visasi na mara nyingi watoto huwa waathirika wakubwa.
Lakini, licha ya wahalifu wengi kutumia
mwanya huo kuwateka watoto ambao hawawezi kujitetea, wakati mwingine
wahalifu hao hufanya hivyo kwa watu wazima pia.
Tukio la hivi karibuni la kutekwa na
kuteswa kwa muuguzi wa Hospitali ya Mwananyamala, Pili Amiri (pichani)
huku watekani wakitoa sharti la kupewa Sh5 milioni ili wamuache huru, ni
mfano wa matukio hayo.
Pili, mwenye umri wa miaka 26, alitekwa
akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala Komakoma, saa tano asubuhi,
Alhamisi ya Machi 12 na kuingizwa katika gari linalodaiwa kuwa ni la
watekaji hao.
Kwa mujibu wa mjomba wa Pili, Rahim
Kangile baada ya tukio hilo watekaji hao walipiga simu wakitumia namba
ya Pili na kudai kutumiwa kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo, matukio mengi ya utekaji
yanajumuisha watoto, mfano Novemba 12, mwaka jana, mtoto Tania Omondi
(5), wa Kenya alitekwa huku watekaji wakitaka kupewa kiasi kikubwa cha
fedha.
Katika tukio jingine, mtoto Kelly
Muthoni (6), alitekwa katika kipindi hichohicho. Kelly alitekwa wakati
wa misa ya Jumapili katika Kanisa la Mavuno Bellevue, Nairobi.
Watekaji walitaka Sh90 milioni na walimrudisha baadaye baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha.
Novemba 2010, mwanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Nairobi, Sarah Aruwa alitekwa nyara na watekaji walitaka kiasi cha
Sh1,800,000.Hata hivyo, Sarah alipatikana akiwa ameuawa.
-Mwananchi
tiko
tiko
Post a Comment