tiko
tiko
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa
Jukwaa
la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi
katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa
na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya “hapana”.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana
na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu
Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki
Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa
la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili
za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya
Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha
mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini
wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu
vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa
wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu
zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.
Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada
ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa
Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge
kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo
hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina
ya viongozi mbalimbali wa dini.
Pia tamko hilo limekuja siku chache
baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya
Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha
mchakato wa Kura ya Maoni.
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo
walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama
wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na
uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.
Katiba inayopendekezwa
Taarifa hiyo ya maneno 712 inasema:
“Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani
imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa
kwa hila na ubabe.
“Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya
wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na
maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na
uwiano wa mihimili ya dola.
“Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa
ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa
dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa
rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi
kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya
tamko hilo.
Mahakama ya Kadhi
Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi,
taarifa hiyo inasema, “Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama
tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari
16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha
kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa
hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua
raia wake kwa misingi ya dini.”
tiko
tiko
Post a Comment