tiko
tiko

Hatima ya tuhuma za Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na wenzake kuhusu fedha walizopata kutoka iliyokuwa akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT), itapelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete.
Ofisa
Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Filotheus Manula, ameliambia
mwandishi kuwa, baada ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma kukusanya tuhuma pamoja na utetezi wa pande zote mbili,
limeandika ripoti na utetezi na kuuwasilisha kwa Rais ambaye ndiye
mwenye maamuzi ya kutoa hukumu.
Alisema
wao wamemaliza vikao vyao na kinachoendelea ni kuandaa ripoti ambayo
baraza hilo litaeleza kwa nini liliamua kumpeleka mshitakiwa ndani ya
baraza na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa pamoja na utetezi wa
watuhumiwa hao.
“Baada
ya kupeleka majumuisho yetu, uamuzi wa hukumu uko kwa Rais kwani baraza
halina uwezo wa kutoa hukumu na ndiyo inavyofanyika kwa miaka yote,”
alisema.
Chenge
alipanda katika kizimba cha Baraza la Maadili, kujibu mashitaka ya
kutumia madaraka yake vibaya alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
kushauri Serikali iingie mkataba wa miaka 20 na kampuni ya IPTL.
Aidha,
anadaiwa baada ya kustaafu wadhifa huo wa uanasheria wa Serikali
Desemba 24, mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa mshauri
mwelekezi wa kampuni wa VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa
na hisa za asilimia 30 kwenye kampuni ya IPTL na kujipatia Sh bilioni
1.6.
Baada
ya kusomewa mashitaka hayo, mbunge huyo alikataa kesi hiyo kusikilizwa
na kuwasilisha pingamizi la kutaka suala hilo kutoendelea kusikilizwa
kwa kuwa tayari kuna kesi ya msingi Mahakama Kuu inayoendelea
kusikilizwa.
Naye
Profesa Anna Tibaijuka, aliitwa katika Baraza la Maadili kwa viongozi
wa umma kujibu tuhuma za kukiuka maadili ya uongozi na kujipatia Sh
bilioni 1.6 ambazo aligawiwa kutoka katika fedha za akaunti ya Tegeta
Escrow.
Hata
hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa
hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo
hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na
kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio
na uwezo lakini wenye vipaji.
Mbunge
wa Sengerema, William Ngeleja, alikiri mbele ya Baraza la Maadili ya
Viongozi wa Umma kwamba, aliomba na Sh milioni 40.4, kutoka kwa James
Rugemalira kwa kujitetea, alifanya hivyo kama ilivyo kawaida pia kwa
wabunge wengine.
Ngeleja
alidai mbele ya baraza hilo kwamba, msaada huo aliopewa na Rugemalira,
hauna tofauti na mingine aliyowahi kupokea kutoka kwa wafanyabiashara
wakubwa kama vile Reginald Mengi, Said Salim Bakhresa na Yusuf Manji.
Wengine
ambao taarifa zao zitapelekwa kwa Kikwete, ni Mnikulu Shaban Gurumo,
Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Rugonzibwa Mujunangoma, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Ufilisi na Udhamini
(RITA), Philip Saliboko, Naibu Kamishna Upelelezi na Kodi Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Loicy Appollo.
Pia
yumo Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Dk
Benedict Diu na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulam
Remtullah.
tiko
tiko
Post a Comment