Askari wa Usalama Barabarani wakiwa wamezikamata baadhi ya pikipiki
ambazo madereva wake wamekutwa na makosa mbalimbali eneo la Mbagala
Rangi Tatu asubuhi hii, ambapo walilazimika kulipa faini ya shilingi
30,000/=
Askari wa Usalama Barabarani wakiendelea na ukaguzi wa bodaboda.
Vijana wakipandisha bodaboda ndani ya gari tayari kwa kuzipeleka Kituo
cha Polisi Maturubai kilichopo Mbagala Kizuiani, Dar.
Askari Polisi wa Usalama Barabarani wakisimamia upandishwaji wa
bodaboda hizo kwenye gari tayari kwa kupelekwa kituo cha polisi.
Askari wa Usalama Barabarani wa jijini Dar-es-Salaam wameanzisha msako
wa kukamata bodaboda zinazokiuka sheria barabarani kama kutovaa kofia
ngumu (helmenti), kupandisha abiria kwa mtindo wa mshikaki, kutokuwa na
leseni za udereva na ubovu wa pikipiki hizo, lengo likiwa ni kuepusha
ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi.
Post a Comment