tiko
tiko
MAHAKAMA Kuu
ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto
Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema
kumjadili, kujadili uwanachama wake na cheo chake ndani ya Chadema,
akikitaka chombo hicho cha sheria kwa kuweka zuio la muda, kusubiri
kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu la Chadema.
Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Richard Mziray, ilikubaliana na
hoja za mawakili wa Chadema waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo
ulikosewa baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa
Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo. Zitto hakufika
mahakamani badala yake alituma mawakili wake.
Wakati Zitto akifungua kesi hiyo Januari mwaka jana, tayari Chadema
ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba
ambao pamoja na Zitto, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi
ya uongozi ndani ya chama hicho. Zitto alikuwa akitetewa na wakili
Albert Msando wakati Chadema iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter
Kibatala na John Mallya. habari hii imethibitishwa na Peter Kibatala.
(HABARI: OJUKU ABRAHAM/GPL)
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment