tiko
tiko
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema analindwa na Mungu na ndiyo
maana chama hicho kimegundua mpango wa mlinzi wake kushawishiwa na
maofisa usalama wa taifa ili kumwekea sumu katika chakula au maji.
Mlinzi huyo (jina tunalihifadhi kwa
sasa) ambaye alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha
Oysterbay juzi, pia anadaiwa kutumiwa na kigogo mmoja wa CCM kuiba siri
za chama hicho.
Tayari polisi imeanza kuchunguza taarifa
hizo na jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura
aliliambia gazeti hili kuwa mtuhumiwa huyo ana haki kama watuhumiwa
wengine wanaofikishwa polisi wakikabiliwa na kesi za jinai na kusisitiza
kuwa; “Tuhuma zinazomkabili ni za kawaida na tunazichunguza.”
Akieleza alivyopokea taarifa hizo Dk
Slaa alisema, “Ninalindwa na Mungu ndivyo ninavyoweza kusema. Chadema
sisi huwa tunaanza na Mungu na kumaliza na Mungu. Ushahidi umewekwa wazi
na hili ni jambo la kweli na limenigusa kwa kiasi kikubwa.”
Alisema baadhi ya mambo yaliyofanywa na
mlinzi wake ameyaona kwa macho na kusisitiza kuwa njama zinazofanywa na
wanaomtumia haziwezi kukiondoa chama hicho katika harakati zake za kila
siku.
“Tupo makini ndiyo maana tumebaini yote.
Tunawajua waliohusika na tupo makini katika kuwafuatilia. Kama Mungu
yupo upande wetu tumuogope nani zaidi,” alisema.
Alisema Chadema ina safari ndefu hivyo
ni lazima wana-Chadema kuvaa viatu ili kujikinga na vumbi na uchafu wa
kila aina, akimaanisha kuwa chama hicho kinakumbana na vikwazo vingi.
Tuhuma dhidi ya mlinzi huyo zilitolewa
juzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando kuwa wamebaini
nyendo za mlinzi huyo na kuzifuatilia kwa ukaribu hadi kupata taarifa
hizo alizosema ni ukweli mtupu.
Hili ni tukio la tatu kwa Chadema kudai
kuna mipango ya kumfuatilia Dk Slaa, mara ya kwanza ilikuwa Februari
2009 alipobaini kutegewa vinasa sauti hotelini mkoani Dodoma na mkakati
uliotajwa kuwa wa kuwaua yeye, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Akieleza jinsi walivyombaini mlinzi
huyo, Marando alisema pamoja na ushahidi wa mawasiliano ya simu, lakini
pia mlinzi huyo alikiri kwa kinywa chake kutumiwa na maofisa hao ambao
hakuwataja majina lakini alisema wako 22.
“Mlinzi alitueleza kwamba alikuwa
akipewa fedha kwa ajili ya kutoa siri za vikao vya chama kupitia simu
yake…kwa kuwa anaruhusiwa kuingia kwenye vikao vya chama hicho kama
mlinzi amekuwa akitegesha simu yake ili kuwapa taarifa watu wa CCM
`live’ ili wasikie kila kinachojadiliwa,” alidai Marando.
Marando aliyewahi kuwa ofisa wa usalama wa taifa na kuongeza kuwa wako mbioni kufikisha suala hilo polisi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment