Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

BREAKING NEWS: Ajali imetokea changalawe Mafinga basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kwenda Dar limeangukiwa na kontena muda huu na watu wengi wanakadiriwa kufariki na hali ni mbaya sana

tiko tiko
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255757438866 / +255756315791. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Ajali imetokea maeneo ya Mafinga mkoani Iringa sehemu inaitwa Changarawe ambapo gari aina lori lilokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya ambapo lilikuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara hadi kupelekea kugongana na basi la abiria mali ya Kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam. Hii ni maelezo ya trafki aliyepo katika eneo la tukio.
Kontena la lori limelalia kabisa basi, na watu wengine wamelaliwa na wengine wameporomokea korongoni, mpaka sasa majeruhi watatu ndio waliopatikana ambao ni watoto wawili makadirio yao ni ya miaka ni mitatu na saba pamoja na mtu mzima ndio wamekutwa wakiwa hai lakini kwa asilimia kubwa watu waliofariki kwenye ajali hiyo ni wengi.
 

Na hawa waliopona inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano uliotokea kati ya basi na roli lililokuwa limebeba Konteina.
Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hapa eneo la tukio unazorota kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi kukosekana Mafinga. Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.



ENDELEA KUTIFUATILIA KWA TAARIFA KAMILI
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top