tiko
tiko

MAISHA ya ndoa na uhusiano wa kimapenzi
ni sanaa yenye umri mkubwa tangu enzi za Adamu na Hawa. Matatizo
yamekuwa ni mengi tangu mwanamke wa kwanza aliyeumbwa kwa ubavu wa
mwanaume alipokubali kudanganywa na nyoka katika bustani nzuri ya Eden
miaka milioni nyingi zilizopita.
Leo hii, sanaa ya mapenzi imeanza
kuingia katika ukisasa, wa kidigitali, kiasi kwamba hata staili tu ya
maisha, inaweza kuwa chanzo cha kustawi au kubomoka kwa ndoa au uhusiano
wa kimapenzi. Kuna ambao kabla ya kuwa pamoja, hawakuwahi kuaminiana,
lakini baada ya kuwa pamoja, wamejikuta katika hali ambayo awali
wasingeweza kuamini.
Katika maisha yetu, tunajuana. Tunajua
jinsi majirani zetu wanavyoishi, hata kama watajaribu kutuonyesha usafi
wa uhusiano wao. Wabantu, hatuna utamaduni wa kuishi kwa wanandoa au
walio katika uhusiano wa kimapenzi kubusiana hadharani, iwe wakati wa
kutoka au kurudi kazini. Lakini baadhi yetu, kutokana na mwingiliano wa
tamaduni, tumejikuta sasa tukiiga uzungu.
Siyo jambo la ajabu leo, mtu na mpenzi
wake kunyonyana ndimi hadharani na yeyote atakayejaribu kushangaa
ataonekana mshamba. Aina yetu ya kusalimiana imebadilika, siku hizi
unambusu mtu shavu la kushoto na kulia, huku mkikumbatiana, hata kama ni
dada, shangazi, kaka, mjomba na kadhalika!
Tabia hizi zimeleta mambo mengi sana, kwani mtu na rafiki yake, wakienda kwa familia rafiki, nao husalimiana kizungu, mke wangu atamkumbatia mshkaji wangu na kumpiga busu, wakati nami nitafanya hivyo hivyo kwa mkewe jamaa!
Tabia hizi zimeleta mambo mengi sana, kwani mtu na rafiki yake, wakienda kwa familia rafiki, nao husalimiana kizungu, mke wangu atamkumbatia mshkaji wangu na kumpiga busu, wakati nami nitafanya hivyo hivyo kwa mkewe jamaa!
Kwa ujumla, siku hizi mke au mume hana
tena uoga wa kumbusu au kumkumbatia mtu asiye wake kwa sababu mbona ni
jambo la kawaida tu, tena linaloweza kufanyika hata mbele yake!
Wapo wanaotumia fursa hii kufanya ufuska wao.
Wapo wanaotumia fursa hii kufanya ufuska wao.
Wanaweza kuwa wana tabia ya kutoka nje
ya ndoa zao, lakini mwenza wake anapohisi kusalitiwa, hutiwa moyo kwa
kuambiwa aache mambo ya kizamani kwani kama ameona alama ya lipstick
shavuni kwa mumewe, ni jambo la kawaida tu kwani alipigwa busu na bosi
wake kazini katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Au kama ni mwanamke, mume anapohisi kitu
katika ukaribu wake na jamaa wa mtaani kwao, ataambiwa aache hayo mambo
watu wasije kumcheka, kwani mke na mume wa mtu kukumbatiana kwenye
pikipiki ni jambo la kawaida na wala vicheko baina yao visimkwaze kwa
sababu wasingeweza kukumbatiana wakiwa wamenuna.
Kitu cha msingi ni kutambua kuwa wapo
wanawake au wanaume wahuni ambao wamezaliwa na tabia hiyo na wengine
hujikuta wakiamua kuwa hivyo baada ya kuchoshwa na wenza wao. Na
ieleweke kuwa maneno kuwa maji hufuata mkondo yana nafasi ndogo sana
katika mapenzi. Yaani eti kwa sababu baba alikuwa ni kiwembe sana basi
na kijana wake atafuata nyayo, no!
Ndiyo maana huwa tunasikia mtoto wa kasisi akisifika kwa ufuska wakati mzazi wake ni mtu wa sala muda wote.
Ndiyo maana huwa tunasikia mtoto wa kasisi akisifika kwa ufuska wakati mzazi wake ni mtu wa sala muda wote.
Lakini pia ni lazima tukubali kuwa kero
za mwenza mmoja zinaweza kusababisha mke au mume kuamua kutoka nje
kutafuta unafuu.Mtu anapokosa amani ndani ya nyumba yake, hutamani
kuipata nje. Ingawa amani haimaanishi kushiriki mapenzi nje ya ndoa,
lakini idadi kubwa ya watu waliokwaruzana na waume au wake zao, huamini
kuchepuka kunapunguza kitu wanachokiita ‘stress’.
Kwa hiyo jambo la msingi sana kuzingatia
kwa wanandoa na walio katika uhusiano wa kimapenzi ni kwamba jitahidi
kadiri unavyoweza, ili usiwe chanzo cha kero kwa mwenzako kwa sababu
ukizidisha, utamfungulia milango ya kwenda kutafuta unafuu nje. Na
elewa, aina yoyote ya maisha ambayo hayampendezi mwenzako ni kero!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment