Kesi
ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba
Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama
ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa
siri.Kesi hiyo ilianza
kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5 hadi saa 8
mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora
Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi
hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na
imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.
Post a Comment