tiko
tiko
MSANII mahiri
wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' amefikisha
mashabiki laki tano (500,000) kupitia akaunti yake katika mtandao wa
kijamii wa Instagram.
Kupitia akaunti yake hiyo ya Intagram, Diamond aliwashukuru mashabiki
wake wanaozidi kumsapoti kula kukicha kwa kuandika maneno yafuatayo:
"Familia siyo tu watu ambao umezaliwa pamoja nao, ila ni pamoja na wale
ambao upo nao saa 24 kwa uzuri au kwa ubaya, ambao wanakupenda au
wanakuchukia. Hiyo ndiyo familia.
Nawapongeza sana wanafamilia wangu wa Instagram kwa kufikia nusu milioni" Aliandika staa huyo.
Kwa sasa staa huyo ndiye msanii mwenye mashabiki wengi katika mtandao Instagram.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment