tiko
tiko
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutolewa hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa baada ya kupoteza fahamu na kisha kupelekwa kituo cha Polisi oysterbay kwa ajili ya mahojiano.
Akiongea
na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi na
kupewa dhamana, Gwajima amesema hawezi kutishika na vikwazo
anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea wakristo nchini .
“Nimetoka
kwa amani, nashukuru sana Mungu ameniponya,ila nasema sitoacha kusema
ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao wanakandamizwa na mifumo ya Katiba
ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
Askofu Gwajima amewataka viongozi wenzake kuheshimu tamko lililotolewa na Jukwaa la Kikristo Tanzania.
“Nawaamomba
viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu Tamko hili la kikristo na endapo
tutakuwa tofauti basi tutakuwa tunapingana na msimamo wetu na mimi
mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho” ameongeza Gwajima.
Alipoulizwa na waandishi wa Habari kuhusu Afya yake Gwajima amesema hawezi kuzungumzia Afya yake kwa sasa.
Kabla
ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika
Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo
kuna daktari wake maalumu.
tiko
tiko
Post a Comment