tiko
tiko
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Serikali imesema asilimia 20 ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ni wazee wenye wenye umri wa kati ya miaka 60 na kuendelea.
Serikali imesema asilimia 20 ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ni wazee wenye wenye umri wa kati ya miaka 60 na kuendelea.
Hayo yalisemwa bungeni leo na Waziri wa
Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista
Mhagama alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum
(Chadema), Conchesta Rwamlaza.
Rwamlaza alisema kwa muda mrefu wazee
nchini wamekuwa wakililia kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi
kama vile Bunge, halmashauri, vijiji kama ilivyo kwa makundi mengine ya
vijana, watu wenye ulemavu na wanawake.
Mbunge huyo alitaka kufahamu ni lini
serikali itasikiliza kilio cha wazee hao na kuweza kuweka utaratibu wa
kuwa na wawakilishi wazee ndani ya Bunge kama ilivyo kwa makundi
mengine.
Akijibu maswali hayo, Mhagama alisema sheria zilizopo hazielezi juu ya kutenga viti maalum katika Bunge.
Hata hivyo, alisema vyama vyenyewe vya siasa vinaweza kuweka nafasi za wazee katika makundi ya watu wenye ulemavu na wanawake.
“Hivi sasa tuna asilimia 20 ya wabunge wazee wenye umri wa kati ya miaka 60 na kuendelea,”alisema.
Alisema wawakilishi wa makundi
mbalimbali bungeni, halmashauri na vijiji mfano wanawake, vijana na watu
wenye ulemavu wamekuwa wakipatikana kupitia mapendekezo yanayowasilisha
na vyama vya siasa.
“Ili kuongeza uwakilishi wa makundi
mbalimbali wakiwemo wazee, vyama vya siasa vinahimiza kuhakikisha
mapendekezo yanayopelekwa kwenye vyombo vya uchaguzi, yanahusisha
makundi mbalimbali ikiwemo kundi la wazee,”alisema.
tiko
tiko
Post a Comment