WAKATI
wimbo wa ‘Hawajui’ wa msanii, Vanessa Hau Mdee ‘Vee Money’, ukiongoza
katika chati za ubora za vituo mbalimbali vya redio na runinga za nchini
Nigeria, msanii huyo amesema wasanii wengi hawajui namna ya kutumia
mitandao ya kijamii kuuza kazi zao.Vanessa
alieleza hayo jana alipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006)
Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The
African, akiwa katika harakati za kutangaza wimbo wake mpya wa ‘No body
but Me’ aliomshirikisha rapa mkongwe KO kutoka Afrika Kusini. Wimbo huo
utaanza kusikika katika vituo vya redio na kuonekana katika runinga
mbalimbali kuanzia siku ya Alhamisi.
Vanessa
amekuwa mfano wa wasanii wanaonufaika na kazi zake kupitia mitandao
mbalimbali, lakini wasanii wengi hawajui namna ya kunufaika nao ndiyo
maana wanaonufaika na kazi hizo za mitandaoni si wasanii wenye kazi zao. “Wasanii
wengi hawajui namna ya kujiandikisha, hawatambui namna ya kuuza kazi
zao kupitia mitandao lakini naamini wapo baadhi ya watu wananufaika na
kazi za wasanii hao mitandaoni bila wao kujua,’’ alisema huku akiwataka
wasanii waweke mazoea ya kujiandikisha katika mitandao hiyo ili
wanufaike nayo “Mimi
nina watu zaidi ya 300,000 wanaofuatilia muziki wangu hivyo zipo
kampuni kupitia nafasi hiyo mitandaoni zinafanyakazi nami kwa malipo
mazuri, pia natumia kampuni hizo kutangaza kazi zao kupitia muziki wangu
nao wananilipa hadi wakati mwingine fedha hizo natumia kwa ajili ya
kuandaa video za nyimbo zangu,’’ alieleza Vanessa.
TUPE MAONI YAKOTUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE!!!.
Post a Comment