tiko
tiko
Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu msimamo wa chama hicho kuunga mkono na kushiriki mgomo uliotishwa na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania(TUCTA, baada ya serikli kushindwa kuteleleza madai ya wafanyakazi
Rais
Jakaya Kikwete ametangaza Aprili 30 kuwa ni siku ya kupiga Kura ya
Maoni, lakini Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinataka kuitumia kwa
malengo tofauti; imepanga kuanza mgomo nchi nzima wa kudai stahiki zao.
Chama
hicho, ambacho kinaongoza walimu shule za msingiu na sekondari wapatao
206,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, kimeeleza kuwa iwapo
Serikali itakuwa haijatekeleza maazimio yao matano ifikapo tarehe hiyo,
walimu watachukua uamuzi mgumu kama ule wa mwaka 2012.
Uamuzi
huo uliofikiwa kwenye mkutano wa Baraza la CWT uliomalizika Morogoro
wiki mbili zilizopita, umekuja katika kipindi ambacho wadau wengi wana
shaka na utayari wa Serikali kufanikisha mchakato wa Kura ya Maoni
kutokana na viashiria vingi vya vikwazo, hasa muda wa kutosha kutekeleza
masuala yote yanayohitajika kama Sheria ya Kura ya Maoni inavyotaka.
Ingawa
Tume ya Uchaguzi (Nec) imeeleza kuwa mambo yote yako sawa kufanikisha
Kura ya Maoni, zikiwamo fedha za kuendeshea mchakato huo, tamko hilo la
CWT linaonekana litakuwa kizingiti kingine kikubwa kwa Serikali, hasa
kutokana na ukweli kuwa walimu ndio hutumika sana kwenye shughuli za
upigaji kura.
Akizungumza
jana, rais wa CWT, Gratian Mukoba alitaja maazimio hayo kuwa ni kuitaka
Serikali kulipa Sh16 bilioni ambazo ni madeni ya walimu, kupandisha
walimu wanaostahili, kulipwa mishahara waliokuwa wanadai tangu mwaka
2012, mwalimu kuwa na mwajiri mmoja kati ya Wizara ya Elimu na Tamisemi
na kubadilishwa kwa kanuni za viinua mgongo kwa wastaafu.
“Yote
haya yanatakiwa kutekelezwa ifikapo Aprili 30 mwaka huu la sivyo Baraza
litawataka walimu kuchukua uamuzi mgumu. Fedha za kumlipa mwalimu zipo,
lakini wanaozifaidi ni wachache,” alisema Mukoba, ambaye pia ni rais wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta).
“Ukisikiliza
mijadala bungeni ni wizi na ufisadi. Mara mishahara hewa... mara
(sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta) Escrow, lakini
walimu hawalipwi wala kutatuliwa matatizo yao. Hii ni kwa sababu
Serikali iliyopo imeshindwa na umefika wakati sasa kuiondoa madarakani.”
Mwaka
2012 CWT ilitikisa nchi baada ya kufanya mgomo nchi nzima ulioungwa
mkono na walimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo na ambao ulisambaa
hadi kwa wanafunzi walioamua kuandamana ili kuishinikiza Serikali
kuwalipa walimu wao.
Mwaka
huo, Julai 27 CWT iliandika notisi ya saa 48 kuhusu mgomo huo, lakini
Serikali ikautangaza kuwa si halali kwa maelezo kuwa unakiuka taratibu
za kimahakama baada ya pande hizo mbili kufikishana Mahakama Kuu,
Divisheni ya Kazi kujaribu kutatua tatizo hilo.
Jana,
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa alisema hawajayapokea maazimio
hayo.
“Wao
wamefikia maazimio hayo, lakini sisi bado hatujayapata na kama
tukiyapata tutawaita na tutazungumza nao,” alisema Waziri Majaliwa
“Mfano
suala la madeni wao watakuwa wamelizungumza kwa ujumla hivyo tukikutana
tutaweza kuwaeleza tumefikia wapi katika utekelezaji wa kila eneo.”
Lakini
Mukoba alipofuatwa kuzungumzia kauli hiyo ya Waziri Majaliwa, alisema:
“Kama anasema hawajayapata, basi wasubiri Aprili 30 kuyapata. Serikali
ina ubabaishaji na kama ndiyo hivyo mwambie asubiri Aprili 30 atayapata
maazimio hayo.”
Aliongeza
kusema:”Kama anasema hawajui mbona watumishi kutoka Tamisemi walikuwa
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wanafuatilia
madeni ya walimu kama hawajui wanachokifuatilia huko ni nini, wasubiri
wataona?”
Nec
ilikuwa imependekeza kutumia wanajeshi katika mchakato wa Kura ya
Maoni, lakini pendekezo hilo limepingwa na wadau, hasa wanasiasa na
wanaharaka ambao wamesema matumizi ya chombo hicho cha dola yatatisha
wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura na pia siku ya kuhitimisha
mchakato huo ambayo ni Aprili 30.
Kwa
hali hiyo, Nec italazimika kutumia walimu kwenye mchakato huo mkubwa na
unaohitaji nguvu kazi kubwa hasa wakati wa upigaji kura.
Tayari
vyama vya upinzani vinavyoundwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
vimetangaza kujitoa kwenye mchakato huo wa Kura ya Maoni, ambao
utahusisha uandikishaji wa wananchi kwenye Daftari la Wapigakura, utoaji
wa elimu kuhusu yaliyomo kwenye Katiba Inayopendekezwa, upigaji wa
kampeni za kutaka wananchi waikubali au waikatae na kuhitimishwa kwa
kupiga kura.
Mchakato
wa Kura ya Maoni imekuwa na vikwazo vingi tangu wakati wa Bunge Maalum
la Katiba wakati vyama vya upinzani vilipodai kuwa chombo hicho kilikuwa
kinapoteza mwelekeo kwa kuacha kujadili Rasimu ya Katiba
iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na badala
yake kujadili rasimu iliyokuwa na utashi wa CCM.
Baadaye
vyama hivyo vikaunda Ukawa na mwezi Aprili vikasusia vikao vya Bunge la
Katiba, na juhudi za kuwarejesha bungeni zilkishindikana.
tiko
tiko
Post a Comment