tiko
tiko
Imeelezwa
kuwa imani za kishirikina ndiyo chanzo cha walimu kushindwa kufundisha
maeneo ya vijijini pindi wanapopangiwa kutokana na kutishiwa maisha
wanapotoa adhabu kwa wanafunzi wao.
Mratibu
Elimu Kata ya Mvomero, Malonga Dilukwili alisema hayo jana
alipozungumza na walimu, maofisa watendaji wa vijiji na madiwani kwenye
mafunzo ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika elimu yaliyoandaliwa
na Asasi ya Elimu na Mazingira (Wetu) mkoani hapa.
“Inasikitisha,
walimu wamekuwa wakijitolea kufundisha lakini wenyeji wanawatolea
maneno ya vitisho kuwa wataondoka. Sasa kwa mtindo huu elimu itapanda
maeneo ya vijijini?” alihoji Dilukwili.
Mkufunzi
wa mafunzo hayo, Dk Joseph Saqware alisema ili elimu ikue maeneo ya
vijijini, ni lazima wazazi na walimu washirikiane katika kukuza sekta
hiyo. Alisema licha ya walimu kuogopa, lakini miundombinu ya shule za
vijijini haikidhi vigezo vya kufundishia wanafunzi.
Aliiomba
Serikali kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya shule hizo, huku
akisisitiza wazazi na walezi kuacha kuwatolea walimu lugha za kutisha.
tiko
tiko
Post a Comment