tiko
tiko
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Aishael Sumari
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Aishael Sumari,
ameshtushwa na idadi ya watoto wanaoshikiliwa kwa muda mrefu katika
mahabusu kuu ya Mkoa wa Kilimanjaro, wakisubiri kesi zinazowakabili
kumalizika ili kuwapa fursa ya kuendelea na masomo waliyokatisha katika
Shule za Msingi na Sekondari.
Sumari
alipigwa ‘butwaa’, jana asubuhi baada ya kuitembelea mahabusi hiyo,
akiwa ameongozana na majaji Amaisairio Munisi, Benedict Mwingwa na
Mahakakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi-Moshi.
Baada
ya kujionea hali halisi ya mahabusu hiyo, iliyopo chini ya Idara ya
Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Kilimanjaro, Jaji Mfawidhi, aliwaambia mahabusu
hao kwamba, mahakama imeguswa na mahitaji yao na kwamba ameuelekeza
uongozi kuwasilisha mara moja kwa Msajili, majina ya watoto wanaosota
mahabusu muda mrefu wakisubiri haki.
“Hapa
siyo mahali mnapostahili kuwapo; tumejifunza ni kwa sababu gani
mmewekwa hapa kwa muda mrefu, ingawa tunajua ni balaa limewapata
tu…tunaamini baada ya haki, mtakuwa waadilifu kwa wazazi na hata jamii
inayowazunguka,” alisema Jaji Sumari.
Aliongeza:
“Nimeuelekeza uongozi wa mahabusu, uniletee majina yenu na kesi
zinazowakabili ili tuone namna ya kuwatendea haki na msiendelee kuitwa
wahalifu kwani sio jambo la furaha kwenu.”
Majaji
hao, Mahakimu na watendaji wengine wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro,
walikwenda kuadhimisha siku ya sheria nchini katika mahabusu hiyo pamoja
na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi kwa kujionea hali halisi na
kisha kugawa zawadi mbalimbali zikiwamo viatu, sukari, ndoo, dawa za
meno, juisi na vifaa vya usafi.
Awali,
akitoa ufafanuzi kuhusu mahabusu hao, Afisa Ustawi wa Jamii (Mfawidhi)
wa kituo cha Moshi, Wolfgang Kimaro, alisema idadi kubwa ya mahabusu
wanaoshikiliwa ni wanafunzi wa Shule za Msingi ambao bila ya msukumo wa
mahakama, wataendelea kusotea haki na kupoteza mwelekeo wa kupata elimu
kama taa ya maisha pamoja na makuzi ya walezi au wazazi wao.
tiko
tiko
Post a Comment