tiko
tiko
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) mwishoni mwa wiki iliyopita kimeadhimisha miaka 38
tangu kuzaliwa kwake katika kaya hii. Mazuri na mabaya yake sitayajadili
leo bali nitaangalia jambo moja nalo ni IMANI.
2015 ni mwaka wa uchaguzi. CCM kama chama tawala kinaingia kwenye kinyan’ganyiro hicho kikiamini falsafa ya ya kiongozi wake wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere kuwa rais bora hawezi kutoka nje ya CCM.
Kwa masikio yangu mimi Mkuu wa Kaya nilimsikia mwenyekiti wa chama hicho taifa, Jakaya Kikwete, akisherehesha imani hiyo alipokuwa anahutubia maelfu ya wafuasi wa CCM katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Najiuliza; imani ya chama hicho tawala
inaambatana na matendo? Maana ni wazi Nyerere aliposema rais bora
atatoka CCM alimaanisha CCM bora siyo dhaifu.
Msingi wa hiki ninachokisema unajengwa na kauli ya muasisi huyo pale aliposema: “Bila CCM imara nchi itayumba.” Hapa ndipo mahali pa kujadili.
Msingi wa hiki ninachokisema unajengwa na kauli ya muasisi huyo pale aliposema: “Bila CCM imara nchi itayumba.” Hapa ndipo mahali pa kujadili.
Je, wakati mwenyekiti wa sasa
akisisitiza imani ya chama chake mbele ya wanachama anaamini kuwa CCM
anayoingoza ni bora kama zama za Mwalimu na kwamba ina sifa za kutoa
rais bora?
Namkumbusha; Kikwete aliposisitiza kuuenzi wosia wa Mwalimu anakumbuka kauli ya muasisi wake aliyosema; Watanzania wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje?
Kwa mawazo ya leo, hakuna asiyejua kuwa kioo cha CCM kimemeguka vipandevipande na taswira zinazoonekana ndani zinatofautiana. Chama kimegawanyika katika makundi.

Leo hii mwenyekiti akisimama mbele ya
kioo cha chama chake haonekani mwili mzima, amegawanyika kiasi cha
kutoutambua utimilifu wake na ndiyo maana anasisitiza ongezeko la
wagombea urais wenye sifa kwa kuwa waliojitokeza hawajaweza kuziba ufa
wa kioo chake.
Mwenyekiti angali anatishwa na kivuli
cha makundi; Nyerere hakuwa mwoga, alikuwa jasiri, mwenye kusimamia
anachokiamini. Waliofanya naye kazi wanashahidisha kuwa hakuongoza kwa
matakwa ya chama bali ya wananchi.
Msingi huu ndiyo ambao CCM inapaswa
kuufuata katika kuelekea kuipatia kaya hii mkuu mpya mwenye sifa ya
ubora. Vinginevyo imani waliyorithishwa kuwa rais bora atatoka CCM
itakuwa haina maana.
Mwananzengo wenzangu; wakati chama hicho kikiadhimisha miaka 38 ya uhai wake, falsafa tatu lazima tuzifikirie sana kwa mustakabali wa kaya hii, nazo ni RAIS BORA KUTOKA CCM, WATANZANIA WANATAKA MABADAILIKO NA BILA CCM IMARA NCHI ITAYUMBA.

Kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu,
lazima wananzengo tujihoji juu uimara wa chama tawala na kama kitaweza
kumteua mgombea bora tunayemtaka. Maana tunaweza kuamini falsafa kuwa
rais bora atatoka CCM lakini wakubwa wakajiteulia mgombea atakayelinda
maslahi yao na sisi tukadanganywa kwa imani iliyokufa na kuzikwa kuwa
rais bora lazima atoke CCM. Tusikubali!
Jambo la pili ni uhitaji wa mabadiliko.
Mgombea ajaye lazima awe na kigezo cha kuiletea kaya hii mabadiliko
ambayo Wanazengo wanayataka. Tukiletewa mgombea ambaye hana sifa hii
tutoke usingizini tuyatafute mabadiliko yetu nje ya CCM!
Mwisho wake ni CCM dhaifu kuiyumbisha
nchi. Kama nilivyosema, chama hiki kutokana na makundi ya urais
yanayonyukana kuingia ikulu, yanaweza kukidhoofisha chama hicho. Hilo
likitokea tusikubali kuyumbisha nchi nzima, badala yake tukiache chama
kiyumbe chenyewe na ikiwezekana kianguke madarakani kabisa!
Huu ndiyo msimamo wangu mimi Mkuu wa Kaya. Shime Wananzengo wenzangu, niungeni mkono katika mawazo haya!
Huu ndiyo msimamo wangu mimi Mkuu wa Kaya. Shime Wananzengo wenzangu, niungeni mkono katika mawazo haya!
tiko
tiko
Post a Comment