tiko
tiko
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi
makubwa kifo cha Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa
Bodi ya BASATA Bw. John Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita
usiku wa kuamkia Ijumaa ya Tarehe 13/02/2014.
Aidha, BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa
Msanii Dully Sykes, Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe
15/02/2015.
Pamoja na vifo hivi kuacha majonzi na huzuni kwa wanafamilia, ni pigo
pia kwenye tasnia ya Sanaa kutokana na ukweli kwamba wote wawili kwa
njia moja ama nyingine wamekuwa na mchango katika kuhakikisha tasnia hii
inasonga mbele kwa kuwa karibu na wasanii John Kitime na Dully Sykes
sawia.
Baraza linatoa pole kwa wadau wote wa Sanaa hususan wasanii na Umoja wa
mabloga nchini kwa misiba hii. Ni matumaini ya Baraza kwamba,
tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu hawa hasa
kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment