tiko
tiko
MTU mmoja,
Mugusuhi Nyarusahe (39) mkazi wa Kijiji cha Kinyambwiga wilayani Bunda,
amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), cha Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kucharangwa visu na wenzake tumboni,
katika kile kilichodaiwa kuwa ni mzozo wa mgawo wa fedha zilizotokana na
mauzo ya ng’ombe, tukio lililotokea wiki iliyopita.
Bw. Mugusuhi Nyarusahe (39) aliyecharangwa kwa visu na wenzake.
Nyarusahe ambaye ni maarufu kwa jina la
Serikali, alipatwa na mkasa huo baada ya kuzuka ugomvi katika baa moja
iitwayo Gateway Bar & Guest House iliyopo Kiabakari wilayani
Butiama.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kundi la watu sita lilifika katika baa hiyo na kujitenga kando mishale ya saa 11 jioni na kuanza kuagiza vinywaji huku wakiwa na mazungumzo yao.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kundi la watu sita lilifika katika baa hiyo na kujitenga kando mishale ya saa 11 jioni na kuanza kuagiza vinywaji huku wakiwa na mazungumzo yao.
Ghafla, watu hao walianza kumwagiana
pombe ovyo vichwani na kuzua taharuki kubwa kwa wateja wengine huku
wakipasua chupa za bia na Mukebha Marwa alichomoa kisu kutoka ndani ya
koti alilokua amevaa na kumchoma Mugusuhi na kusababisha utumbo
kumwagika chini.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema watu hao walikuwa wakibishana juu ya mgawo wa fedha zilizotokana na mauzo ya ng’ombe wanaosadikika kuwa wa wizi.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema watu hao walikuwa wakibishana juu ya mgawo wa fedha zilizotokana na mauzo ya ng’ombe wanaosadikika kuwa wa wizi.
Akizungumza akiwa hospitalini, Mugusuhi
alisema ameanza kujitambua baada ya kuzirai tangu alipochomwa kisu na
kwamba baada ya kukatwa utumbo mara tatu na kushonwa ameanza kupata
nafuu “Mungu atanisaidia nitapona,” alisema.
Jeshi la polisi kupitia kwa msemaji wake
Kamanda ASP Alex Kalangi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na
kueleza kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
tiko
tiko
Post a Comment