tiko
tiko
BONDIA bingwa
wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka ambaye juzi alihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kumpiga mtu ngumi,
alihenyeshwa kiasi cha kutosha kabla ya kupandishwa kwenye karandinga la
Magereza lililompeleka kuanza maisha mapya katika gereza la Manispaa ya
mkoa.
Awali, baada ya hukumu hiyo, Cheka alipelekwa katika chumba ambacho mahabusu hukaa kusubiri kuondoka na akiwa huko, alionekana akikabidhi baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwa ndugu na jamaa zake.
Awali, baada ya hukumu hiyo, Cheka alipelekwa katika chumba ambacho mahabusu hukaa kusubiri kuondoka na akiwa huko, alionekana akikabidhi baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwa ndugu na jamaa zake.
Bondia bingwa wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka akiwa chini ya ulinzi mkali.
Wakati akiondolewa kwenda kupanda gari,
Cheka alichukua simu yake na kuwapigia baadhi ya marafiki zake
kuwajulisha juu ya msala huo, lakini Polisi hawakumruhusu kuendelea na
jambo hilo, kwani walimnyang’anya na kumpeleka garini, ambako aliungana
na mahabusu pamoja na wafungwa wengine.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa Cheka
waliokuwepo mahakamani hapo, waliangua kilio baada ya hukumu hiyo,
akiwemo mkewe ambaye inasemekana kuwa ni mgonjwa. Mdogo wake naye
aliangua kilio kikubwa kiasi cha kusaidiwa na meneja wa bondia huyo.
Cheka akichukuliwa na mahabusu wengine kwenye karandinga kwenda kuswekwa lupango.
Wakizungumzia hukumu hiyo, baadhi ya
wakazi wa mjini hapa walisema Cheka aliichukulia kirahisi kesi hiyo na
ndiyo maana amehukumiwa, kwani tokea kuanza kwake, hakuwahi kupeleka
shahidi na hata siku ya hukumu, alishindwa kutoa utetezi wowote.
tiko
tiko
Post a Comment