tiko
tiko
Baada ya
usiri wa muda mrefu, bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma
Namusoma ameamua kumuweka hadharani mkewe na mototo wake na hivyo kuzima
zile tetesi kuwa Ostaz ni msela tu asiye na mke wala mtoto.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook, Ostaz Juma ameweka picha ya mkewe ajulikanaye
kwa jina la Mariamu Daudi au mama Hayyan akiwa pamoja na mtoto wao wa
kiume, Hayyan Juma.
Sambamba na picha hizo, Ostaz alisindikiza na maneno yasemayo:
“For
those who didn't know that I have a wife and a kid, let it be known
now...kwamba mimi nina mke na mtoto, nampenda sana mke wangu (mary
david) na nampenda sana mwanangu hayyan boy hayyan juma. namuomba sana
mungu atuhifadhi na maadui wa kibinadamu na wasio jua thamani ya familia
ya mtu, eeh mola mjaalie mke wangu maisha marefu na afya na amani ya
moyo wake na utulivu, utupe watoto wengine zaidi ya huyu, aamiin,
nakupenda sana mke wangu popote utakapo kua ikumbuke familia yako”.
Kuibuka
kwa Ostaz kumekuja wakati kukiwa na ukimya kuhusu kampuni yake
aliyoianzisha ya kuendeleza vipaji vya wasanii ya Mtanashati
Entertainment ambayo miaka miwili iliyopita iliibuka kwa kasi na
kumrudisha tena kwenye game msanii PNC, kuwapa sapoti akina Mkude Simba
na marehemu Sharo Milionea.
Akizungumzia
ukimya wa Mtanashati, Ostaz alidai kuwa kampuni yake haijafa na haiwezi
kufa ila kwa uwezo wa Mungu na kusema kuwa hivi sasa ana dili na
wasanii wachanga na soon atafanya surprise kubwa katika tasnia ya Bongo
Fleva!
tiko
tiko
Post a Comment