tiko
tiko
Wananchi
hao waliokuwa na hasira wamesema hakuna sababu ya kuwa na mwenyekiti
ambaye wananchi hawamkubali kwa sababu katika uchaguzi uliopita kulikuwa
na udanganyifu katika upigaji kura,kutokana na hali hiyo wamesema ni
bora kuachana na vyama vya siasa wachague mwenye kiti wa kimila ili
kukisaidia kijiji cha puma kupata maendeleo.
Baada
ya vurugu kuongezeka diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM,Bwana
ramadhani kulungu ilibidi kufunga kikao hicho ili kuweza kumnusuru
mwenyekiti wa kijiji cha puma na kuwatuliza wananchi ilikusitokee
uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti
wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM ,Bwana Sifa Joramu awali ambaye
alishindwa kabisa kuendesha kikao chake ,baada ya jeshi la polisi
kuingilia kati na kuamua kumsindikiza kwa ulinzi mkali huku wananchi
waki mzomea na kusema hawamtaki,amesema hizo ni fujo za vyama vya
upinzani lakini yeye atahakikisha kazi anafanya kwa sababu yeye ndiye
aliyeshinda na kuapishwa kwa kazi ya uwenyekiti wa kijiji cha puma.
Kundi
la watu waliamua kumfuata na kumbeba juu kisha kumzungusha mitaani
Bwana Hassan Chaimbo aliye gombea kwa tiketi ya CHADEMA na kushindwa kwa
kupata kura mianne arobaini na nne dhidi ya Bwana Sifa Joramu
alishinda uwenyekiti wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM katika
uchaguzi uliofanyika mwishoni mwaka jana na kupata kura mianne hamsini
na saba.
tiko
tiko
Post a Comment